Diamond ampa mfanyikazi wake zawadi ya gari na kipande cha ardhi siku ya harusi yake

Ambangile ni miongoni mwa wafanyakazi wa #SportsArena ambao huandaa kipindi cha kila wiki cha michezo kwenye Wasafi FM.

Muhtasari

• Hili ni gari la pili ambalo Ambangile atapokea kutoka kwa bosi wake Chibu Dangote. 

Diamond amzawadi mfanyikazi wake George Ambangile gari jipya na kipande cha ardhi
Diamond amzawadi mfanyikazi wake George Ambangile gari jipya na kipande cha ardhi
Image: INSTAGRAM

Mwishoni mwa wiki, mkuu wa WCB na Mkurugenzi Mtendaji wa Wasafi Media, Diamond Platnumz alimzawadia mmoja wa wafanyakazi wake gari jipya kabisa na kipande cha ardhi.

George Ambangile ambaye ni mtangazaji wa michezo katika kituo cha Wasafi FM alifanya harusi na mpenzi wake Lilyan Komba na bosi wake Platnumz ni miongoni mwa waliopamba hafla hiyo maalum.

Wakati wa hotuba yake na sherehe ya harusi, Diamond aliwatakia wawili hao ndoa njema kabla ya kuweka hadharani zawadi yake kwa Ambangile na mkewe.

“Sisi kama timu ya Wasafi, tunakupa zawadi ya kipande cha ardhi ... na pia kesho hakikisha umemwona meneja wangu wa fedha Don Fumbe ili aweze kukubadilisha gari hilo," Diamond alisema.

Hili ni gari la pili ambalo Ambangile atapokea kutoka kwa bosi wake Chibu Dangote. Mnamo Aprili 2021, George Ambangile alipata gari jipya la Toyota Crown, kwa kazi hii ya mfano katika Wasafi FM.

Katika chapisho, kituo hicho kilisema kwamba Mkurugenzi Mtendaji wao aliona hitaji la kumthamini Ambangile kwa kuwa bora miongoni mwa wafanyakazi wa #SportsArena ambao huandaa kipindi cha kila wiki cha michezo kwenye Wasafi FM.

Ambangile sasa ameongeza jina lake kwenye orodha ya watu waliozawadiwa magari na mwimbaji Diamond Platnumz.

Kati yao; Mtangazaji wa Wasafi TV Aaliyah, Comedian Coy Mzungu, Zuchu, Mbosso, Lala Lava, Harmonize, aliyekuwa Mpiga Video Lukamba, Mama Dangote, Majidi Ramadhani aka Bravesty (WCB Wasafi Social Media Manager), Juma Lokole na kaka wa kambo wa Alikiba Issaa Azam.