Amber Ray amnunulia mtoto wake Iphone 14 kusherehekea kufikisha miaka 13

Ray alificha kadi zenye matakwa mawili na kumtaka mwanawe kuchagua moja kati ya ziara ya kwenda Paris Ufaransa au kununuliwa simu ya Iphone 14

Muhtasari

• "Karibu kwenye ujana mwanangu @gavinclassic,” Ray alisema.

Amber Ray amnunulia mwanawe zawadi ya Iphone 14.
Amber Ray amnunulia mwanawe zawadi ya Iphone 14.
Image: Instagram

Siku moja iliyopita mtoto wa mwanamitindo Amber Ray kwa jina Gavin alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa kufikisha miaka 13.

Kama mama mzazi mwenye furaha kuona alichokikuza kwa miaka 13, Amber Ray ambaye ni mjamzito wa mtoto wa pili alimtaka Gavin kufanya chaguo moja kati ya matamanio mawili ambayo aliandika kwenye kadi mbili na kuficha maandishi yake kwa kutumia kiganja chake.

Matamanio hayo yalikuwa kuchagua kati ya kujishindia ziara ya kwenda Ufaransa, jiji kuu la Paris au kununuliwa simu ya Iphone 14 pro max.

“Kama unavyojua ni siku yako ya kuzaliwa, sasa nataka ufanye chaguo moja kati ya kadi hizi mbili zenye matamanio,” Amber Ray alianza kumwambia Gavin.

Gavin ambaye alikuwa ameketi kwenye kochi akishiriki mchezo kwenye simu alifanya chaguo la tamanio la pili ambalo lilikuwa la kununuliwa simu ya Iphone.

Mara hiyo hiyo waliondoka nyumbani na kwenda hadi kwa duka la kuuza simu za Iphone ambapo Ray alitekeleza tamanio la mwanawe huku akimkaribisha kwenye ujana.

“Maisha ni mchezo wa kuchagua, na kadi unazoacha nyuma huwa sababu ya chaguzi zako zinazofuata. Kazi yangu kama mama yake ni kumtengenezea mazingira ambayo chaguzi zake ni bora tu kwa bora na kutoka bora. Karibu kwenye ujana mwanangu @gavinclassic,” Ray alisema.

Mama kijacho anatarajia kuzaa mtoto wa pili hivi karibuni ambaye ujauzito unakadiriwa kuwa wa Kennedy Rapudo.

Wiki chache zilizopita wapenzi hao wawili walidokeza kuachana lakini pia wamekuwa wakionekana pamoja, jambo ambalo linazidi kuzua mchanganyiko mwingi kwa wanaowafuatilia wasiweze kujua kama kweli wameachana ama ni kiki tu za kutafuta umaarufu ambao tayari wako nao.