Tanasha Donna atathmini kuhama Kenya akidai ni taifa la fujo tupu

Donna alisema kuwa japo Kenya kuna maendeleo ya kupigiwa mfano lakini kila siku tangu mwaka kuanza ni lazima kitu kibaya kitokee.

Muhtasari

• Awali Donna amewahi nukuliwa akisimulia kwa kina kuhusu familia yake ambayo haijulikani na wengi.

Image: INSTAGRAM// TANASHA DONNA

Aliyekuwa mtangazaji na mzazi mwenziwe wa Diamond Platnumz, Tanasha Donna amedokeza kukosa furaha nchini Kenya na anatathmini kuhama kwenda mataifa ya nje pamoja na mtoto wake kabisa wasiweze kurejea tena.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Donna ambaye ni mama wa mtoto mmoja alilalamika kwamba mwaka huu tangu uanze nchi inasonga mbele vizuri katika mambo mengine lakini kila mara lazima kuna kitu hasi ambacho kitatokea.

Alisema kuwa anaendelea mchakato wa kukusanya kila kilicho chake akiwemo mtoto wake na kuhama kabisa, bila kutaja atakwenda taifa gani.

“Sitaki kudanganya, taifa hili ni fujo tupu. Ninajaribu kukusanya kile kilicho change pamoja na mwanangu na mizigo yangu na kuondoka kabisa tena kwa uzuri. Ni fujo tupu kwa sababu huwa tunasonga ndio lakini sasa kila siku tangu 2023 ianze lazima kuna kitu kibaya kitatokea. Kenya ni nini kinaendelea?” Tanasha Donna aliuliza.

Awali Donna amewahi nukuliwa akisimulia kwa kina kuhusu familia yake ambayo haijulikani na wengi.

Msanii huyo alisema kwamba mama yake anaishi Ubelgiji.

Mama huyo wa mtoto mmoja alizaliwa nchini Uingereza kwa baba wa Kiitaliano na mama Mkenya, lakini baadaye alihamia Kenya, ambako alikaa kwa muda kabla ya kuhamia Ubelgiji, ambako alilelewa na baba yake wa kambo kutoka Ubelgiji.

“Watu wanaponiuliza ninatoka wapi, sijui nianzie wapi. Nilizaliwa Uingereza, nilikulia Kenya kisha nikahamia Ubelgiji, lakini baba yangu mzazi ni Muitaliano na baadhi ya mchanganyiko huko, lakini nilikua na baba wa kambo wa Ubelgiji," aliandika.