Samidoh avunja kimya baada ya mkewe kupakia picha akiwa na mwanajeshi wa Marekani

Edday, ambaye anafurahia likizo na watoto wake katika nchi hiyo ya Magharibi, alishiriki picha hiyo huku akiwasalimu mashabiki wake.

Muhtasari
  • Wanamitandao wengi walidai kana kwamba anamkejeli mkewe kwa methali hiyo inayotoka au kusemwa na watu wa loitoktok.
Samidoh, Edday Nderitu, na mwanajeshi wa Marekani
Image: HISANI

Saa chache baada ya mkewe kupakia picha kwenye mtandao wake wa kijamii akiwa na mwanajeshi wa Marekani, mwimbaji wa Mugithi Sammy Muchoki almaarufu Samidoh amevunja ukimya kwenye mitandao yake ya kijamii.

Wanamitandao wengi walidai kana kwamba anamkejeli mkewe kwa methali hiyo inayotoka au kusemwa na watu wa loitoktok.

''Mwanamke anayeruhusu watu kuonja chakula chake kabla ya kununua huishia kulisha kijiji kizima bila kuuza sahani ~ Kimana -Methali ya Loitoktok,'' Samidoh alichapisha.

Edday Nderitu saa chache zilizopita alioakiapicha akiwa na mwanajeshi wa Marekani ambaye hakufahamika jina lake huku picha hiyo ikisambaa mitandaoni na wengi wakimpongeza wakimtaka kutafuta mapenzi nje ya nchi.

Edday na Samidoh wamekuwa na matatizo ya ndoa baada ya mwimbaji huyo kuhusika na seneta mteule Karen Nyamu akiwa na watoto wawili naye.

Nyamu hajamuonea huruma mama wa watoto watatu. Amekuwa akianika uhusiano wake na msanii Mugithi.

Edday, ambaye anafurahia likizo na watoto wake katika nchi hiyo ya Magharibi, alishiriki picha hiyo huku akiwasalimu mashabiki wake.

Baadhi ya wanamitandao walionekana wakimshauri mama huyo wa watoto watatu kumtema Samidoh na kubaki na mwanajeshi huyo.

Wengine walidai kuwa Edday ana ladha ya wanaume waliovalia sare kwani mbali na muziki, Samidoh pia ni afisa wa polisi.

Mwaka jana, mwimbaji huyo wa Mugithi ambaye ni afisa wa Polisi wa Utawala alisema hajapata sababu ya kuacha kazi ya polisi licha ya mafanikio yake katika tasnia ya muziki. Mara nyingi yeye hushiriki picha na video zake akitumbuiza katika sehemu mbalimbali za dunia lakini si akitoa huduma za afisa wa polisi.

"Ninafanya kazi siku za wiki na inapohitajika pamoja na kipindi cha wikendi huwa nafanya muziki wangu, kama talanta nyingine yoyote katika huduma ya polisi," alisema katika mahojiana na Word Is.