Muonekano mpya wa Lupita baada ya kutuma ombi la kuigiza kwenye filamu mpya

Kwa muda mrefu mashabiki wa mshindi huyo wa Tuzo za Oscar wamemzoa kuwa na rasta lakini safari hii aliibuka kichwa bila nywele.

Muhtasari

• Lupita Nyong'o alishiriki katika ukurasa wake wa Instagram picha yake akiwa amenyoa upara na kuonyesha furaha ya mwanzo mpya bila nywele.

Lupita Nyong'o aibuka na mwonekano mpya wa upara.
Lupita Nyong'o aibuka na mwonekano mpya wa upara.
Image: Instagram

Muigizaji maarufu wa Hollywood Lupita Nyong'o, ameibuka na muonekano mpya akiwa bila nywele miezi minne baada ya kumtambulisha mpenzi wake muongozaji filamu Selema Masekele mwenye umri wa miaka 51. 

Katika picha hiyo mpya, mshindi huyo wa Tuzo la Oscar mwaka wa 2014 alidhihirisha furaha yake na kutaja muonekano wake kuwa mwanzo mpya baada ya wengi kumzoea na nywele za rasta kwa muda mrefu.

Binti huyo wa Gavana Nyong'o alidokeza kwa mashabiki wake kwamba alishrutika kunyoa nywele zake za kichwa baada ya kutuma maombi ya kuigiza kwenye filamu mpya ya Dora Milaje.

"Nina furaha kutokelezea bila nywele, tayari nimeshatuma maombi ya kuigiza kwenye filamu ya Dora Milaje," Lupita alisema kwa mbwembwe. 

Mashabiki wake kwenye mtandao wa Instagram walimpongeza kwa kupata muonekano mpya kichwani wengine wakimtakia kila la kheri katika kupata nafasi ya kuigiza kwenye filamu hiyo.

"Malkia wetu huyo," aliandika msanii kiongozi wa bendi ya Sauti Sol, Bien Baraza na kumalizia na emoji za mapenzi.

"Umenipa ujasiri zaidi wa kukubali na kukumbatia hali yangu ya sasa," aliandika Themamamiax.

"Nywele ni nyongeza tu ambayo unapendeza ndani na nje, na bila 💝  ," mwingine alimhongera.

Kando na uigizaji, Nyong'o anaunga mkono uhifadhi wa kihistoria kwani anazungumza kuhusu kuzuia unyanyasaji wa kijinsia, kufanya kazi kwa haki za wanawake na wanyama.

Binti wake Gavana wa Kisumu Anyang' Nyongo pia aliandika kitabu cha watoto kwa jina Sulwe ambacho kilikuja kuwa nambari moja kwa muuzaji bora wa New York Times.