Kwa nini Gidi amekosa kusafiri kuhudhuria kuhitimu kwake USA na 'birthday' ya bintiye Ufaransa

Mtangazaji huyo alijilaumu kwa utepetevu alioufanya huku akisema kuwa amepata funzo kubwa.

Muhtasari

• "Mshtuko juu yangu, visa yangu ilikuwa imeisha na sikujua. Na hivyo ndivyo nilivyokosa kuhitimu kwangu huko Texas na siku ya kuzaliwa ya binti zangu huko Ufaransa,” Gidi alisema.

Gidi afichua sababu za kutosafiri kwenda Marekani na USA kama alivyopanga.
Gidi afichua sababu za kutosafiri kwenda Marekani na USA kama alivyopanga.
Image: Maktaba

Mtanazaji Gidi amefichua sababu ya kutosikika Jumatatu ya Mei 15 katika kipindi cha asubuhi katika kituo cha Radio Jambo.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Gidi alifichua kwamba yuko kwenye siku zake za likizo na alikuwa na mipango ya kusafiri kwenda Marekani kuhudhuria kuhitimu kwake.

Pia, Gidi alikuwa na mipango ya kusafiri kwenda Ufaransa kushuhudia binti yake akiongeza mwaka mwingine maishani.

Lakini kwa bahati mbaya, mipango hii yote imebuma, kulingana na mtangazaji huyo.

Gidi alisema kuwa alikuwa ameweka kila kitu tayari kwa ajili ya safari hiyo lakini hakuwa amejua kuwa visa yake ya usafiri ilikuwa imemaliza muda wake wa kutumika, na hivyo ilimbidi kughairisha safari hiyo.

“Niko kwenye likizo yangu ya kila mwaka. Nilikuwa nimekata tiketi ya ndege kwa ajili ya likizo kwenda Marekani kupitia Uingereza na Ufaransa. Ni ibada yangu ya kila mwaka. Safari ilikuwa Ijumaa iliyopita. Mshtuko juu yangu, visa yangu ilikuwa imeisha na sikujua. Na hivyo ndivyo nilivyokosa kuhitimu kwangu huko Texas na siku ya kuzaliwa ya binti zangu huko Ufaransa,” Gidi alisema.

Hata hivyo, mta ngazaji huyo nguli alisema kuwa hawezi kuwalaumu ubalozi wa Marekani kwani ni kosa lake kutojua kuwa Visa yake ilikuwa imemaliza muda wa matumizi na ilihitaji kufanywa upya.

“Pasipoti yangu bado iko kwenye Ubalozi wa Marekani kwa ajili ya kufanya visa upya. Siwezi kuwalaumu, ni kosa langu. Angalia visa hizi za muda mrefu kila wakati. Somo nimelipata kwa njia ngumu,” Gidi alisema kwa kujuta.

Mtangazaji huyo mara kwa moja husafiri kwenda Ufaransa kuona binti yake ambaye anaishi na mamake huko.

Miezi michache iliyoita, Gidi kupitia ukurasa wake wa TikTok alipakia video binti yake akijaribu kumfunza maneno ya kawaida kwa lugha ya Kifaransa.