Mike Sonko awachangamsha mashabiki kwa kuanika pesa hadharani

"Pesa niko nazo ni za kuharibu na bibi zangu, wacha nikuoneshe pesa, wewe unajua maana ya pesa wewe,” Sonko

Muhtasari

• Katika video hiyo, Sonko alionekana ndani ya nyumba yake huku akifoka vikali kwenye video kwa mtu ambaye anadaiwa kumdhihaki kwamba hana pesa.

Sonko aonesha kiburi cha pesa Twitter
Sonko aonesha kiburi cha pesa Twitter
Image: Twitter

Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko amekuwa gumzo mitaani baada ya video yake kuvujishwa akionyesha bunda la pesa zikiwemo noti za kigeni. 

Katika video hiyo, Sonko alionekana ndani ya nyumba yake huku akimfokea vikali kwenye video mtu ambaye anadaiwa kumdhihaki kwamba hana pesa na amefilisika.

Ili kujibu madai hayo ya kufilisika, Sonko aliamua kujibu vikali kwa kuwatembeza mashabiki wake akiwaonyesha makasha ya pesa.

Katika video hiyo ambayo tayari inatamba mitandaoni, Sonko alionekana akifungua makasha na kuanza kutoa dola za thamani isiyojulikana na, muda mfupi baadaye, noti za Kenya, ambazo alisema zilikuwa shilingi milioni mbili.

“Ati sina pesa sababu eti sisaidii watoto, nani amekuambia eti mtu ako na miaka 18 kwenda juu ni mtoto, mtu amezaa? Pesa niko nazo ni za kuharibu na bibi zangu, wacha nikuoneshe pesa, wewe unajua maana ya pesa wewe,” Sonko alisema. 

Alisema kuwa pesa hizo za Kenya ambazo ni shilingi milioni mbili zilikuwa nyumbani na ni pesa ya mfukoni kwa ajili ya mafuta ya gari.

“Hii ni pocket money ya mafuta na Mungu akitangulia kukuchukua wewe nitakununulia jeneza nikuzike huko Embu,” Sonko alisema.

Wakenya katika mitandao ya kijamii walitamaushwa na kiasi hicho cha pesa, huku baadhi yao wakijiuliza mahali Sonkoree anatoa pesa. 

“Mike Sonko anapata wapi pesa zake 🤔😢 anaishi kama prime publo escobar,” Mmoja alisema.

“Mike Sonko ndio sababu mimi husema kila mara kuwa Mwanaume ana mantiki TU wakati ana pesa ZAIDI,” Mwingine alisema.