Rappa Ssaru awapoteza wanafamilia wa karibu naye

Msanii wa muziki wa kizazi kipya 'Sipangwingwi' amefiwa na binamu zake wawili

Muhtasari
  • Hii ni kwa sababu kwa bahati mbaya alipoteza wawili wa wanafamilia wake wa karibu, jambo ambalo limeuacha moyo wake vipande vipande.
Sylivia Ssaru
Image: Facebook

Rapa na mwimbaji mashuhuri wa Kenya Sylvia Ssaru almaarufu Ssaru yuko kwenye majonzi baada ya kupoteza wanafamilia wa karibu naye.

Hii ni kwa sababu kwa bahati mbaya alipoteza wawili wa wanafamilia wake wa karibu, jambo ambalo limeuacha moyo wake vipande vipande.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya 'Sipangwingwi' amefiwa na binamu zake wawili, na alitoa habari hiyo ya kusikitisha kwa wafuasi wake wa Instagram Jumatatu ya tarehe 15 Mei.

Hii ilikuwa kupitia chapisho kwenye hadithi zake za Instagram, ambapo Ssaru alishiriki kwamba wawili hao walikufa kifo cha kusikitisha pengine wakiwa pamoja.

"Nimepoteza wanafamilia wawili wa karibu mara moja chini ya hali mbaya sana. Moyo wangu umepasuka 😣. Siwezi hata kufikiria jinsi shangazi yangu na marafiki wa karibu na jamaa wanahisi hivi sasa.

Hakuna kifo bora lakini bado naamini hamkustahili kufa hivyo 💔. Mpumzike kwa amani binamu 🕊😭" aliandika rapper huyo.

Kutoka kwa chapisho hilo ni wazi kuwa Ssaru hakuwahi kufichua majina ya binamu wapendwa na hata hakuwahi kutoa maelezo ya jinsi walivyoaga dunia.