Njugush azungumzia ukweli kuhusu picha yake kuwa kwenye kitabu cha kemia

Alisema kuwa picha hiyo ilipigwa alipokuwa akifanya karatasi ya kemia, mtihani wa mwisho shule za Upili, KCSE.

Muhtasari

• Njugush alisema kuwa somo la Kemia ni miongoni mwa masomo magumu sana shuleni, na ndilo lililomfanya asifikie ndoto zake,

• Aliamua kufanya somo la Kemia na sayansi zingine zote kwa sababu alitaka kuwa rubani.

Njugush afichua jinsi picha yake ilijipata kwenye kitabu cha kemia.
Njugush afichua jinsi picha yake ilijipata kwenye kitabu cha kemia.
Image: Facebook

Mmoja wa waundaji wa maudhui maarufu na maarufu na pia mcheshi mtandaoni, Njugush hivi karibuni katika odkasti moja alifunguka, jinsi alivyojikuta kwenye Jalada la Kitabu cha cha Kemia cha shule ya upili.

Akizungumza katika kipindi cha podikasti na Mwafreeka, Njugush alikiri kwamba mtu ambaye yuko kwenye jalada la kitabu hicho ni yeye, na bado anakumbuka wakati picha hiyo ilipigwa.

Alisema kuwa picha hiyo ilipigwa alipokuwa akifanya karatasi ya kemia, mtihani wa mwisho shule za Upili, KCSE. Kisha akapakia picha hiyo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Na hivyo ndivyo mmoja wa marafiki zake wenye weledi wa kufanya ukanganyifu kwenye picha hiyo na kuiweka kwenye kitabu cha kemia.

“Hipi picha ni yangu lakini hiyo kitabu nafikiria waliwekelea tu. Kuna jamaa pale Twitter anakuwa mnoma sana mambo ya graphics, ndio alifanya huo utaalamu,” Njugush alisema akimsifia jamaa huyo.

Alishtuka kwa sababu hakutarajia hilo kutokea. Njugush alisema kuwa somo la Kemia ni miongoni mwa masomo magumu sana shuleni, na ndilo lililomfanya asifikie ndoto zake, ambazo zilikuwa ni kufaulu masomo yote ya sayansi na kuwa rubani.

“Picha hiyo nilipigwa nikiwa karatasi ya mwisho ya kemia, nilikuwa napenda sana Kemia. Nilikuwa nataka kuwa rubani na nikachukua sayansi zote, kemia wakati ilianza kuchanganyikana na hesabu ndio tulianza kuchanganyikiana kwa sababu mbona nifanye hesabu kwa kemia?” Njugush alijiuliza.

Mcheshi huyo alikiri kwamba akiwa katika shule ya upili chochote kilichohusisha hisabati, kilikuwa tatizo kubwa sana kwake, kwa ujumla alikuwa akichukia hesabu, na labda hiyo ndiyo sababu iliyomfanya asifaulu kupata alama alizotaka katika KCSE.

Hata hivyo alisema kuwa anashukuru kwamba anafanya mema, na ubunifu wa maudhui pia umemfanya kuwa mkubwa, na kwa sasa anaishi maisha yake ya ndoto.