Prince Indah akutana na shabiki wake mkubwa ambaye pia ni mfanyikazi wa nyumbani

Jumatano Indah na Adhis hatimaye waliweza kupatana kwa mara ya kwanza.

Muhtasari

• Mwanamke huyo kwa jina Adhis Marwa awali alikuwa amechapisha video akisema kuwa atanunua deta kutazama nyimbo za Prince Inda.

 

Msanii Prince Indah na Adhis
Msanii Prince Indah na Adhis
Image: INSTAGRAM

Mwanamziki wa mitindo ya Ohangla Evans Ochieng almaarufu Prince Indah hatimaye amekutana na mfanyikazi wa nyumbani ambaye awali alikuwa umemuonyesha upendo wa dhati.

Mwanamke huyo kwa jina Adhis Marwa awali alikuwa amechapisha video akisema kuwa atanunua data bundles ili kutazama nyimbo zote za msanii huyo.

Video hio ilimvutia Indah na akawaomba mashabiki wamsaidie kumpata mwanamke huyo.

Indah baadaye aliweza kupata namba yake ya simu na kumnunulia data jambo ambalo Adhis alilithamini sana.

Jumatano Indah na Adhis hatimaye waliweza kupatana kwa mara ya kwanza.

Adhis alijawa na furaha baada ya kukutana na mwanamziki huyo na hata kupata fursa ya kupiga picha naye.

Indah aliweka video katika akaunti yake ya Tik Tok iliyowaonyesha wakisakata densi pamoja.

Je, wewe ungejihisi aje kupatana na msaanii unayemuenzi?