Mwanafilamu maarufu Abel Mutua amenunua gari jipya aina ya Land Rover Discovery 4.
Abel amekuwa akiendesha gari aina ya Mercedes Benz E250 ambalo amemiliki kwa Zaidi ya miaka .
Katika video iliyoichapishwa kwenye akaunti ya Instagram ya rafiki yake Eddie Butita, Abel alionekana mwenye furaha tele huku akikagua gari hilo.
Katika video hiyo Eddie Butita anaonekana kumkejeli rafiki wao wa thati Njugush kuwa gari hilo la kifahari ni bora zaidi kuliko gari la Njugush.
"Timothy Kimani Ndegwa usiongee na mimi. Ukitaka kuzungumza na mimi andika barua pepe na nitakujibu ndani ya siku tatu hadi tano za kazi. Kimani kwisha wewe," Abel alimtania Njugush.
Kabla ya video hiyo ya gari lake jipya kuibuka, awali Mutua alikuwa amechapisha kwenye mtandao na kutangaza kuwa analiaga gari lake la zamani la Mercedes Benz.
Baba huyo wa mtoto mmoja aliandika ujumbe wa huzuni ulioambatana na video ya gari hilo likiwa limepakiwa kwenye lori.
Alilishukuru gari hilo kwa kumbukumbu za thamani na kumtumikia kwa miaka mingi.
Alikuwa amelipa jina la utani gari hilo Miss GT (God’s time)
"Na baada ya miaka mitano ya kupendeza, ni wakati wa kukuaga. Hili lilikuwa mojawapo ya magari bora zaidi ambayo tumewahi kuwa nayo. Kwa kweli inahisi aina fulani ya njia, lakini, lakini ujue, Mabadiliko hayaepukiki. Naomba Miss GT apate mmiliki mzuri kwa maana anastahili. Mlisema stage ya Kiambu ilihama pale Park Road ama nirisk tu?" aliandika mwigizaji huyo.