Mercy Kyallo athibitisha uvumi kuwa yeye na dada yake wamewai kukosana

Mercy Kyallo alisema kuwa wanablogu walikuwa sahihi walipoandika kuhusu ugomvi baina yake na Betty Kyallo.

Muhtasari

• Alieleza kua ugomvi baina ya mandugu ni jambo la kawaida na kua licha ya hayo, uhusiano wake na dada yake Betty Kyallo ipo imara.

• Hata hvyo Mercy hakufichua chanzo cha ugomvi huo lakini alisema kuwa kuna muda walilaazimika kupata ushauri nasaha ili kuwaweza kuongeleshana.

Betty Kyallo na dada yake Mercy Kyallo.
Betty Kyallo na dada yake Mercy Kyallo.
Image: INSTAGRAM

Mercy Kyallo ambaye ni dadake mwanahabari Betty Kyallo, amethibitisha uvumi uliokuwa ukienea mitandaoni kuwa wawili hao walikuwa na mzozo baina yao.

Akizungumza na mpasho News katika hafla ya uzinduzi wa msimu wa pili wa shoo ya Kyallo Culture, alisema kuwa wanablogu walikuwa sahihi walipoandika kuhusu ugomvi baina yake na dadake mkubwa.

“Uvumi uliokuwa ukienea haukuwa uongo, tulikuwa na kutoelewana kwa kipindi fulani cha maisha yetu kama ilivyo kawaida baina ya mandugu na familia zote ninazozijua,”Mercy alisema.

Hata hvyo Mercy hakufichua chanzo cha ugomvi huo lakini alisema kuwa kuna muda walilaazimika kupata ushauri wa maridhiano ili waweze kupatana.

“Shoo hii imetusaidia pia kuweza kutafuta ushauri nasaha ili tuweze kuongeleshana tena baada ya kukosana, Msimu huu wa pili utawachorea taswira halisi ya ugomvi unaokuwa baina ya madada”

Alieleza kua ugomvi baina ya mandugu ni jambo la kawaida na kua licha ya hayo, uhusiano wake na dada yake Betty Kyallo ipo imara.

“Tatizo lililopo pekee ni kuwa tunafahamika na wakenya wengi ndio maana swala hili linakua jambo kubwa, lakini ukweli ni kuwa kila familia hupitia changamoto hizi za mandungu kukosana,” aliongeza Mercy.

Msimu huu wa pili unazinduliwa baada ya msimu wa kwanza wa Kyallo Culture kuonyeshwa  kwa mara ya kwanza miaka miwili iliyopita.