Nilikuwa najigamba najua kubusu hadi nikakutana na Fantana, mtoto alinimeza - Diamond

Msanii huyo alifunguka kuwa alikuwa anajitapa kuwa mpiga busu bora lakini kwa kiwango cha Fantana, haingii hata kidogo.

Muhtasari

• Diamond alienda hatua Zaidi na kuelezea Zaidi jinsi busu la Fantana lilimkosha na kulitaja kama moja ya busu malum kabisa.

• Msanii huyo alifunguka kuwa alikuwa anajitapa kuwa mpiga busu bora lakini kwa kiwango cha Fantana, haingii hata kidogo.

Diamond Platnumz akimbusu Fantana kwenye kipindi cha Netflix.
Diamond Platnumz akimbusu Fantana kwenye kipindi cha Netflix.
Image: Screengrab//YouTube

Siku chache baada ya msimu wa pili nwa mwendelezo wa Young, Famous na African kupeperushwa hewani rasmi na kampuni ya Netflix, gumzo kubwa liikuwa lile la msanii Diamond Platnumz akibusiana kwa mahaba moto na msanii kutoka Ghana, Fantana.

Baada ya video hiyo wakikulana busu kusambaa, msanii huyo sasa amevunja kimya huku akikiri kuwa kabla ya busu la Fantana, hakuwahi pata mrembo mwenye ni fundi katika kula denda kama mlimwende huyo wa Ghana.

Diamond alienda hatua Zaidi na kuelezea Zaidi jinsi busu la Fantana lilimkosha na kulitaja kama moja ya busu malum kabisa.

Msanii huyo alifunguka kuwa alikuwa anajitapa kuwa mpiga busu bora lakini kwa kiwango cha Fantana, haingii hata kidogo.

Alisema kuwa Fantana sit u alimbusu bali pia alihisi kama anamnyonya ulimi.

"Nilifikiri mimi ndiye mpiga busu bora zaidi hadi nikambusu Fantana. Hakuwa akinibusu tu; alikuwa akinimeza. Lilikuwa busu bora zaidi kuwahi kutokea kwangu,” Simba alikiri kwenye video ambayo sasa imeenea mitandaoni.

Wikendi iliyopita baada ya kipindi hicho kutoka, Zari alimkoromea vikali Diamond kwa kile alisema kuwa alikwenda na kudanganya kuwa Zari alikuwa anambembeleza kupata angalau mtoto wa tatu na yeye.

Zari alisema kuwa hajawahi kumtegemea Diamond kwa kitu chochote Zaidi ya karo ya shule kwa watoto wao wawili ambao walipata naye kabla ya kuachana mwaka 2018.

Ari alizidi kujitapa akisema kuwa yeye ni tajiri wa kujitengeneza na wala hakuwahi kutegemea Diamond kumfanya tajiri kwani kitambo hata kabla ya kukutana na kupendana tayari yeye alikuwa bilionea.