Mwanasoka wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba, amkaribisha mtoto wa 3 pamoja na mkewe

“Al Hamdullilah © mwanachama mpya wa Pogba amewasili. Najivunia Malkia wangu" - Pogba alisema.

Muhtasari

• Haijulikani ni lini wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza, hata hivyo walionekana wakiwa pamoja Los Angeles katika majira ya joto 2017.

• Hii ilikuwa ni wakati uleule ambapo Pogba alishiriki katika Kombe la Kimataifa la Mabingwa (ICC) nchini Marekani kwa Man Utd.

Pogba na mkwe wakaribisha mtoto wa tatu.
Pogba na mkwe wakaribisha mtoto wa tatu.
Image: Instagram

Kiungo wa Juventus, Paul Pogba, na mkewe, Zulay, wamemkaribisha mtoto wao wa tatu.

Mwanasoka huyo alisambaza habari na picha zake, mkewe na mtoto mchanga kwenye akaunti yake ya Instagram Jumatano usiku.

Aliandika, “Al Hamdullilah © mwanachama mpya wa Pogba amewasili. Najivunia Malkia wangu * #zulaypogba nina furaha sana #Daddyofthree”

Paul Pogba amekuwa kwenye uhusiano wa muda mrefu na mwanamitindo Maria Zulay Salaues.

Maria alizaliwa huko Robore, Bolivia, kwa hivyo utaifa wake ni wa Bolivia na wengi wamekuwa wakimjua Zaidi kupitia kuwa mchumba wa mchezaji huyo ambaye aliwahi kukipiga Manchester United.

Haijulikani ni lini wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza, hata hivyo walionekana wakiwa pamoja Los Angeles katika majira ya joto 2017.

Hii ilikuwa ni wakati uleule ambapo Pogba alishiriki katika Kombe la Kimataifa la Mabingwa (ICC) nchini Marekani kwa Man Utd.

Taarifa zinazofungamana na hizo ni kwamba mwezi mmoja uliopita, mchezaji wa Brazil anayezipiga klabuni PSG, Neymar Jr pia alitangaza kutarajia mtoto wake wa kwanza na mpenzi wake Bruna Biancardi.

Mwanasoka huyo wa Brazil, 31, na mshawishi wa mitandao ya kijamii, 28, walishiriki chapisho la pamoja kwenye kurasa zao za Instagram kufichua habari zao za kufurahisha.

Neymar tayari ni baba wa mtoto wa kiume Davi Lucca, 12, na mpenzi wake wa zamani na mwanamitandao ya kijamii Carolina Dantas.

Wapenzi hao walipakia msururu wa picha za kupendeza zinazoonyesha mtoto mchanga wa Bruna akichanua, huku Neymar akimpapasa na kumbusu tumbo lake.