Fahyma aonesha hamu kubwa ya kumzalia Rayvanny mtoto wa pili baada ya kurudiana

Wapenzi hao wana mtoto mmoja aliyezaliwa miaka kama 7 iliyopita na wamerudiana hivi majuzi.

Muhtasari

• Rayvanny kipindi hichi anazidi kupambana vikali dhidi ya aliyekuwa mpenzi wake Paula kwa kutumia picha yake pasi na kuridhia kwake.

Fahyma aonesha nia ya kumzalia Rayvanny mtoto wa pili.
Fahyma aonesha nia ya kumzalia Rayvanny mtoto wa pili.
Image: Instagram

Kuna uwezekani mkubwa katika uvumi wa hivi karibuni kwamba baada ya kurudiana, wapenzi Rayvanny na Fahyvanny wana mpango wa kumletea mtoto wao wa pekee Jayden, mdogo wake.

Hii ni kutokana na kile ambacho mpenzi huyo wa Rayvanny aliandika kupitia ukurasa wake wa Instagram, kipande cha Instastory ambapo aliweka picha ya mtoto asiyejulikana ni wa nani na kuonesha tamanio lake kubwa la kupata mtoto wa pili akisema, “Ni muda mwafaka sasa” akiweka pia emoji za mapenzi.

Baadhi ya mashabiki wake wanahisi kwamba Fahyvanny alikuwa na maana kwamba ni muda sasa wa kupata mtoto wake wa pili, miaka takribani saba tangu alipopata mtoto wa kwanza na Rayvanny.

Wapenzi hao wawili wamerudiana hivi karibuni na wapo pamoja katika kisiwa cha malavidavi na ni kipindi ambapo mitandaoni hakukaliki baada ya Rayvanny kutoa tamko la onyo kwa aliyekuwa mpenzi wake Paula na mama yake dhidi ya kutumia picha yake kwenye kipindi chao cha uhalisia cha Beyond the gram.

Ikumbukwe kwamba baada ya Rayvanny kuachana na Fahyvanny mwaka 2019, alisemekana kuzama kwenye huba na binti wa Kajala, Paula lakini mapenzi yao hayakuenda sawa na wakafika muda mwaka jana wakaachana na mwaka huu Rayvanny akarudi kwenye mama wa mtoto wake.

Katika kipindi cha uhalisia cha Beyond the gram, Paula alizungumzia hivi majuzi kwamba kipindi anatoka kimapenzi na Rayvanny, alikuwa bikira na msanii huyo wa Next Level Music ndiye alimtoa usichana wake, huku wakitumia picha yake kuonesha uhalisia.

Lakini Rayvanny hakufuraishwa na kitendo hicho na kufoka vikali akiwataka kutotumia picha zake bila ridhaa yake.

Paula alijibu mipigo vikali akimtupia Rayvanny cheche lakini muda huo wote, Fahyvanny alionekana kusimama upande wa mumewe na kumhakikishia mapenzi tele.