logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Vybz Kartel aripotiwa kushambuliwa na ugonjwa wa kutishia maisha gerezani

Staa huyo wa Dancehall amekuwa na matatizo kadhaa ya kiafya kwa miaka mingi.

image
na SAMUEL MAINA

Burudani01 June 2023 - 07:25

Muhtasari


  • •Kartel  anaugua ugonjwa wa Graves ambao ukiunganishwa na magonjwa mawili ya moyo anayodaiwa kuwa nayo inafanya hali yake ya sasa "kutisha maisha".
  • •Alikowekwa kizuizini mwimbaji  Adidja Palmer almaarufu Vybz Kartel  hana hewa safi, hana maji, na ndoo ya choo.

Mwimbaji maarufu wa Dancehall Vybz Kartel ambaye amefungwa gerezaji anaugua ugonjwa wa Graves ambao ukiunganishwa na magonjwa mawili ya moyo anayodaiwa kuwa nayo inafanya hali yake ya sasa "kutisha maisha".

Haya ni kwa mujibu wa mahojiano ya kipekee kwenye mtandao wa New York FOX5NY ambapo wakili wake alikiri hali ya mwimbaji huyo.

Isat Buchanan, wakili anayemwakilisha Vybz Kartel alimwambia mtangazaji Lisa Evers wa FOX5 New York, kwamba mwimbaji huyo mnamo Jumatatu Mei 29 alikuwa mgonjwa sana.

Alikuwa amemtembelea gerezani. Kartel yuko kizuizini masaa 23 kwa siku kwa madai ya mzozo wa simu ya rununu. "Hali ya Bwana Palmer inatishia maisha,” Buchanan alisema kwa uchungu.

Mtangazaji alimwambia wakili huyo kwamba FOX5NY ilipata karatasi za mgonjwa kutoka kwa daktari binafsi wa Vybz Kartel, mtaalamu wa magonjwa ya viungo, Karen Phillips, ambazo zilieleza kuwa nyota huyo wa Dancehall amekuwa akiugua ugonjwa wa Graves kwa miaka saba na kwamba licha ya kutibiwa, bado haujapona. .

Alikowekwa kizuizini mwimbaji Kartel mwenye umri wa miaka 47, ambaye jina lake halisi ni Adidja Palmer hana hewa safi, hana maji, na ndoo ya choo.

“Shingo yake ilikuwa imevimba. Ukifikiria shati iliyo karibu inchi 18.5 kwenye eneo la shingo, huwezi kuifunga kola kwenye shingo yake, na ndivyo ilivyo mbaya wakati huu… Uso wake umevimba. Na jambo lingine: Yeye huvaa glasi kila wakati; katika hali hii, hiyo husababisha macho yake kutokeza nje,” Buchanan alisema


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved