Natumia Bangi kujituliza - Davido

Davido alisema kuwa bangi humsaidia kupunguza mawazo.

Muhtasari

• Mshindi  huyo wa tuzo za Mwanamuziki bora Africa alisema kuwa dawa hiyo ya kulevya humsaidia kutulia baada ya matatizo ya kila siku.

• Katika mahojiano haya hayo aliongeza kuwa mkewe Chioma alimlenga walipopatana kwa mara ya kwanza.

Msanii kutoka Nigeria Davido.
Msanii kutoka Nigeria Davido.
Image: Instagram

Mwanamuziki maarufu David Adeleke anayefahamika kama Davido alisema kuwa yeye hutumia bangi ili kumsaidia kupunguza msongo wa mawazo.

Davido katika mahojiano na mwanablogu wa Nigeria Tayo Aina alisema kuwa yeye hutumia bangi licha ya dawa hiyo ya kulevya kupigwa marufuku katika nchi ya Nigeria.

Mshindi  huyo wa tuzo za Mwanamziki bora Africa alisema kuwa dawa hiyo ya kulevya humsaidia kutulia baada ya matatizo ya kila siku.

“Navuta bangi, ili kuweza tu kutulia, inachukua muda mrefu kuweza kutulia na mara nyingi mwili wangu hunikumbusha kuwa nimechoka kabla nipumzike,”  Davido alisema.

Davido miaka iliyopita alishutumiwa na mashabiki wake baada ya kuchapisha video akivuta bangi siku mbili baada ya kushiriki ibada katika kanisa la Redeemed Christian Church mjini Lagos.

Katika mahojiano haya hayo aliongeza kuwa mkewe Chioma alimpuuza walipopatana kwa mara ya kwanza.

Davido alipoulizwa angekuwa akifanya nini kama sio kuimba alisema kuwa angekuwa mchekeshaji kwa kuwa alijihisi akiwa mcheshi sana.

“Ningekuwa mchekeshaji kwa kuwa mimi ni mcheshi sana, ata nikiwa shule nilikuwa nawachekesha wanafunzi wenzangu sana na hio iliniwezesha ata sasa kwa muziki wangu kuwa mtu wa watu,”

Mwanamziki huyo alimpoteza mwanawe mwaka jana mwezi wa Novemba na kujitokeza kwa mara ya kwanza katika tamasha za mwisho ya kombe la dunia baada ya kifo cha mwanawe wa pekee, Ifeanyi.

Msanii huyo hata hivyo amerudi hivi majuzi kwa kishindo na kuachilia albamu yake yenye nyimbo 17, Timeless na ambayo inazidi kupata mapokezi ya kishujaa.