Akothee amsherehekea balozi wa Akothee Safaris Sandra Dacha

Akothee alisema anamchukulia Sandra kama mtoto wake.

Muhtasari

• Kulingana na mama huyo wa watoto watano, Sandra ndiye aliyewaalika wageni wote katika harusi yake.

• Akothee alichapisha ujumbe katika Instagram yake akielezea jinsi Sandra ameweza kumsaidia katika biashara yake na sasa

Mjasiriamali Akothee wakiwa na Sandra Dacha.
Mjasiriamali Akothee wakiwa na Sandra Dacha.
Image: INSTAGRAM

Mwanamziki maarufu Esther Akoth almaarufu Akothee amemmiminia sifa balozi wa kampuni yake ya usafiri Akothee Safaris, Sandra Dacha.

Akothee alichapisha ujumbe katika Instagram yake akielezea jinsi Sandra ameweza kumsaidia katika biashara yake na sasa anamchukulia ama mtoto wake.

Mshindi huyo wa tuzo la mwanamziki bora wa kike katika ukanda wa Afrika Mashariki alisema kuwa awali kabla ya kufahamiana na Sandra ilikuwa vigumu kwake kumuamini na ilimlazimu mtoto wake Vesha Okello kumshawishi.

“Kutokana na wanawake kwenye maisha yangu niliogopa kuhusiana na mtu yeyote, watu niliojuana nao baada ya kupata umaarufu waliniumiza na kunifanya nikose kuwaamini wanawake wanaonizingira,”   

Licha ya Akothee kukuwa bado hajapatana na Sandra, Vesha alimchukua Sandra na kumfanya balozi wa kampuni la Akothee, Akothee Safaris.

Mjasiriamali huyo alisema kuwa Sandra ndiye aliyehusika kwa mipango ya harusi yake ya hivi majuzi kwa mume wake mzungu, Denis ‘Omosh’ Shweizer.

Kulingana na mama huyo wa watoto watano, Sandra ndiye aliyewaalika wageni wote katika harusi yake.

“Sandra alipanga harusi yote yeye peke yake, akawaalika wageni wote waliofika katika hio harusi.”

Harusi hiyo ambayo ilikuwa na wageni kathaa mashuhuri kama vile mke wa kiongozi wa upinzani Idah Odinga, mbunge wa Lang'ata Jalang''o, sosholaiti Kabi Wa Jesus pamoja na mke wake na masosholaiti na wanablogu wengine wengi.

Licha ya mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 43 kukejeliwa mitandaoni baada ya harusi yake kwa mzngu huyo aliweka wazi kuwa hana majuto yoyote ya kufunga pingu za maisha na Omosh.