Boyz II Men: Ratiba kamili ya tamasha la Stanbic Yetu - saa kumi Jumamosi hadi cheee!

Milango katika Uhuru Gardens itafunguliwa saa kumi alasiri Jumamosi Juni 10 na tamasha litaendelea hadi alfajiri ya Jumapili Juni 11.

Muhtasari

• Kati ya saa kumi hadi saa moja jioni, mtangazaji G-Money ataongoza awamu ya burudani ya kuwakaribisha watu akiwa na wacheza santuri DJ Forest na DJ Shark.

Kundi la Boyz II Men kukanyaga Kenya kwa mara ya kwanza kwa hisani ya Stanbic Yetu Festival.
Kundi la Boyz II Men kukanyaga Kenya kwa mara ya kwanza kwa hisani ya Stanbic Yetu Festival.
Image: RADIO JAMBO.

Huku njia zote zikiwa zinaelekea katika bustani ya Uhuru, huko Lang’ata kaunti ya Nairobi kwa tamasha kuu la Stanbic Yetu linalofadhiliwa na benki ya Stanbic kwa ushirikiano na kampuni ya Radio Africa, ratiba kamili ya tamasha hilo imetolewa.

Tamasha hilo litafanyika Jumamosi ya Juni 10 na kamati ya maandaizi imetoa program rasmi jinsi mambo yatakavyotokea kwenye hafla hiyo ambayo kwa Zaidi ya miezi miwili sasa imekuwa ndio gumzo la mijini na vijijini kote Kenya.

Kundi la tangu jadi la muzki aina ya R&B kutoka Marekani, Boyz II Men watakuwa wanafunga kazi katika jukwaa huku wakipewac shavu na kundi la muziki kutoka Kenya ambalo limejivunia tuzo nyingi za kimuziki kwa takribani miaka 20, Sauti Sol.

Milango ya bustani ya Uhuru, itafunguliwa majira ya saa kumi alasiri Jumamosi Juni 10.

Kati ya saa kumi hadi saa moja jioni, mtangazaji G-Money ataongoza awamu ya burudani ya kuwakaribisha watu akiwa na wacheza santuri DJ Forest na DJ Shark.

Saa moja kamili kundi la Sauti Sol litajitupa mzima mzima kwenye jukwaa na kutumbuiza makumi ya ngoma zao pendwa kwa takribani saa moja na dakika 30 hadi majira ya saa mbili na nusu usiku.

Wakati huu, macho yote yataelekezwa katika jukwaa ambapo kundi la Boyz II Men litaingia jukwaani na kukiwasha hadi majira ya saa nne usiku – kuwapakulia mashabiki miziki yao ambayo wengi wanaitambua ikivuma enzi za makuzi yao.

Tafrija ya tamasha lenyewe itashika kasi kuanzia saa sita usiku wa manane hadi majira ya majogoo, alafajiri ya saa tisa Jumapili, ambapo wengi watakuwa wameshiba burudani na kuruhusiwa kuondoka kujipanga kwa wiki mpya.

Boyz II Men, Stanbic Yetu Festival.
Boyz II Men, Stanbic Yetu Festival.