Kamene Goro ageuka mbogo akijibu swali kuhusu idadi ya wanaume aliotoka nao kimapenzi

" Ni vibaya sana kuniuliza swali kama hilo wakati mume wangu ameketi hapa kando yangu." - Goro alisema.

Muhtasari

• "Nakuomba unipe heshima sawa na ile ambayo nimekupa leo. [Huyu] amenibooh,” Kamene alisema 


Kamene Goro akasiriswa na swali kuhusu idadi ya wanaume aliochumbiana nao.
Kamene Goro akasiriswa na swali kuhusu idadi ya wanaume aliochumbiana nao.
Image: Screengrab// YouTube

Kamene Goro amecharuka vikali mithili ya mbogo baada ya mwanabogu kutaka kujua kuhusu idadi ya wanaume ambao ametoka nao kimapenzi.

Katika video ambayo imeenezwa mitandaoni, Goro na mume wake DJ Bonez walikwua wanazungumza na wanablogu wakati mmoja alitaka kujua kama alidhihakiwa mitandaoni miaka michache iliyopita alipoweka wazi kipindi hicho akiwa hewani kuhusu idadi ya wanaume ambao amewahi toka nao kimapenzi.

Goro kwa uso uliotandwa hasira kote, alimtaka mwanablogu huyo kumpa heshima yake kama mke wa mtu.

“Siwezi nikazungumzia vitu kama hivyo sasa, naomba mnipatie heshima kama mke wa mtu. Na pia ni vibaya sana kuniuliza swali kama hilo wakati mume wangu ameketi hapa kando yangu. Nakuomba unipe heshima sawa na ile ambayo nimekupa leo. [Huyu] amenibooh,” Kamene alisema kwa kughadhabishwa.

Mumewe DJ Bonez aliunga mkono matamshi yake kwa kusema kwamba watu wanapaswa kuzingatia siku zijazo na sio zamani na kuongeza kuwa ana maisha mabaya ya zamani kama DJ lakini amedhamiria kusonga mbele.

Wawili hao pia walikanusha kuwa hawana hela baada ya baadhi ya watu kusema kuwa waliamua kufanya harusi ya faraghani ambayo haikuvuma sana kutokana na ufukara.

“Ulikuwa ni wakati wa kufurahisha sana. Na watu ambao tulihisi walikuwa wa maana kwa safari yetu ya mapenzi ndio pekee tuliowaalika. Hatukuona haja kualika dunia mzima na kuna watu walikuwa wanasonya,” alisema Goro. “Kwa hiyo sisi hatukuwa tunashindana na watu. Tulifanya harusi vile sisi tunataka wenyewe na tuliridhika. Kwani tunaonekana kufilisika?” Bonez aliongezea kwa kuuliza.

Miaka michache iliyopita wakiwa katika kikao cha mazingira yaliyoonekana kama ni klabu cha starehe, Kamene aliwaambia Andrew Kibe na Prezzo kwamba mpaka kufikia kipindi hicho alikuwa ametoka kimapenzi na wanaume 27.