logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanamke kama si mrembo kama Amber Ray ni heri ninyonge - Oga Obinna

“Ukiangalia Amber Ray, hata hajahangaika kupata mwanaume kama Pritty Vishy." - Obinna.

image
na Davis Ojiambo

Burudani16 July 2023 - 10:45

Muhtasari


  • • Bonez alimpa chaguo mbadala kwamba achukuliwe katika mawazo yake anafaa kumchagua kati ya Pritty Vishy na Akothee.
  • • Obinna alisisitiza kwamba hawezi kumfikiria mtu mwingine kando na Amber Ray.
Obinna akiri kumtolea macho ya tamaa Amber Ray.

Mchekeshaji Oga Obinna kwa mara nyingine ameonesha macho yake ya tamaa kwa mwanasosholaiti Amber Ray akisifia umrembo wake licha ya kufahamu fika kwamba Ray sasa hivi ni mke wa mtu – Kennedy Rapudo.

Katika podkasti yao ya kila Ijumaa usiku, Obinna alisema kuwa kila mwanamume ako na ndoto na taswira ya kufikirika kuhusu yule mwanamke ambaye angetamani kuwa naye.

Obinna alitolea mfano kwa wanamitindo wa humu nchini akisema kuwa haka kama mtu ni mwenye sura mbaya aje akiwa na yeye, lakini kwa akili yake anafunga macho tu na kujifanya kuwa amemuona Amber Ray.

“Ukiangalia Amber Ray, hata hajahangaika kupata mwanaume kama Pritty Vishy. Kila mwanamume, kule yule mtu unafunga macho, kama sasa mimi nafunga macho hivi hata kama ukikuwa ni Pritty Vishy nafunga macho na kuchukulia kama ni Amber Ray. Kati ya Ray na Vishy, mimi nachukua Ray. Hata kama Vishy ako na ujasiri mimi sitaki hiyo nataka mwili wa Amber Ray, nataka tabasamu lake, rangi yake, vidole vyake, minenguo yake,” Obinna alisema.

Bonez alimpa chaguo mbadala kwamba achukuliwe katika mawazo yake anafaa kumchagua kati ya Pritty Vishy na Akothee.

Obinna alisisitiza kwamba hawezi kumfikiria mtu mwingine kando na Amber Ray na kama kweli chaguo ni hizo mbili tu basi ni heri ajishughulikie mwenyewe kujiridhisha kimapenzi.

“Ni Amber Ray” Obinna alisisitiza, “Amber Ray hayuko, ni kati ya Pritty Vishy na Akothee,” Bonez alimkatisha, “Wacha ninyonge,” Obina aijibu huku Kamene akishindwa kuzuia kicheko chake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved