logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Maikrofoni Cardi B anadaiwa kumtupia shabiki yapigwa mnada kwa milioni 14 Ebay

Maikrofoni ilivutia zaidi ya zabuni 120 kabla ya kuuzwa.

image
na Davis Ojiambo

Burudani09 August 2023 - 12:43

Muhtasari


  • • Kulingana na nakala ya Jarida la Forbes, bidhaa hiyo ilivutia watu wengi katika mnada wa mtandaoni kufuatia urushaji maikrofoni.
Card B.

Kipaza sauti ambacho msanii wa Marekani Card B alidaiwa kumtupia shabiki mmoja na kumjeruhi nacho mwishoni mwa mwezi Julai kimeripitiwa kupigwa mnada kwa kima cha takribani shilingi milioni 14 pesa za Kenya [$99000].

Kwa mujibu wa taarifa mbali mbali, maikrofoni hiyo iliwekwa sokoni na watu mbali mbali wakawasilisha dau la kutaka kukinunua ili kuwa kweney historia ya kumiliki kipaza sauti hicho.

Kufikia Jumanne, ilidaiwa kwamba mtu mmoja alikuwa ametoa dau la kiasi hicho cha pesa kwenye mtandao wa mauzo ya kidijitali, e-Bay ili kukinunua.

Kulingana na nakala ya Jarida la Forbes, bidhaa hiyo ilivutia watu wengi katika mnada wa mtandaoni kufuatia urushaji maikrofoni uliotangazwa sana. Maikrofoni ilivutia zaidi ya zabuni 120 kabla ya kuuzwa.

Mnamo Julai 29, wakati akitumbuiza katika Klabu ya Ufukweni ya Drai’s huko Las Vegas, mshiriki mmoja wa watazamaji alimrushia kinywaji rapper huyo ambaye alijibu kwa kurusha kipaza sauti chake kwenye watazamaji.

Inasemekana kipaza sauti kilimpiga mwanamke ambaye aliwasilisha ripoti ya polisi. Cardi B baadaye aliorodheshwa kama mshukiwa wa kesi ya kuzua rabsha kwenye tafrija.

Uchunguzi wa jinai ulizinduliwa kuhusu tukio hilo lakini baadaye ukatupiliwa mbali kwa sababu ya ushahidi wa kutosha.

Video za sakata ya kurusha maikrofoni zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na ilidaiwa kwamba Cardi B ndiye aliwataka mashabiki wake kumrushia maji ya chupa wakati anatumbuiza jukwaani.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved