logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mbona Ibraah amekaa kimya muda mrefu bila kutoa muziki? Harmonize amejibu

“Tunamalizana na Zaka (Zikki) na Chinga anarudi kwa kishindo cha aina yake."

image
na Davis Ojiambo

Burudani09 August 2023 - 12:16

Muhtasari


  • • Alisema uongozi unaendelea kushughulikia utata ulioibuka baina ya Zikki na Ibraah kwa kushikilia ngoma zake pamoja na ripoti zote za maokoto.
  • • Harmonize hata hivyo aliwapa matumaini mashabiki wa Ibraah kwamba hivi karibuni anarejea katika ubora wake.

Kwa mara ya kwanza, mkurugenzi mtendaji wa lebo ya Konde Music Worldwide Harmonize amefichua sababu kuu ya msanii wake wa pekee aliyekwama naye mpaka sasa Ibraah, kukaa kimya.

Ibraah amekawia sana kuachilia miziki mipya kwa takriban mwaka mzima sasa na mashabiki wake wengi wamekuwa wkiibua maswali kutaka kujua mbona ukimya na kama kila kitu kiko sawa upande wake.

Harmonize wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwenye Instagram Jumanne, mmoja alimuuliza kuhusu suala hilo na msanii huyo alijibu akisema kwamba hana tatizo na Ibraah katika konde Gang balo matatizo yake yametokana na jukwaa la kusambaza miziki kwa njia ya kidijitali, Zikki.

Harmonize hata hivyo aliwapa matumaini mashabiki wa Ibraah kwamba hivi karibuni anarejea katika ubora wake.

Alisema uongozi unaendelea kushughulikia utata ulioibuka baina ya Zikki na Ibraah kwa kushikilia ngoma zake pamoja na ripoti zote za maokoto.

“Tunamalizana na Zaka (Zikki) na Chinga anarudi kwa kishindo cha aina yake. Wamezuia mapato yake pamoja na ripoti za maokoto kwa miezi minane sasa bila sababu yoyote. Serikali inalifanyia kazi suala la Ibraah na najua mnasubiri sana ujio wake,” Harmonize alisema.

Ibraah ndiye msanii pekee ambaye mpaka sasa amesalia katika lebo ya Harmonize, ikiwa ni miaka michache baada ya kusaini kwenye lebo hiyo.

Wasanii wengine ambao walikuwa wamesaini naye ni pamoja na Anjella, Killy na Chiddi ambao wote mpaka sasa wamegura lebo hiyo na kumuacha Ibraah akiwa anashikilia.

Kwa mwaka mmoja uliopita, Ibraah amekuwa mkimya bila shughuli yoyote, jambo ambalo limewapa wasiwasi mashabiki wake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved