logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jacque Maribe atangaza kurejea kwenye media, "Likizo imekamilika!"

“Karibu tena malkia,” mchekeshaji DJ Shit alisema.

image
na Davis Ojiambo

Burudani16 August 2023 - 08:33

Muhtasari


  • • Jaji Idris Nzioka aliyeketi katika Mahakama ya Sheria ya Milimani katika uamuzi wa Machi, alisema kwamba Maribe na Jowie wana kesi ya kujibu.
Jacque Maribe

Mtangazaji wa zamani wa runinga ya Citizen Jacque Maribe amedokeza kurejea kwenye kazi ya vyombo vya habari ikiwa ni miaka kadhaa baada ya kuwa mbali.

Maribe kupitia ukurasa wake wa Instagram alipakia ujumbe wa kudokeza kwamba hatimaye likizo yake ndefu imefikia kikomo na hivi karibuni – pengine kuanzia Septemba mosi – atafanya ujio upya kwenye vyombo vya habari.

“Tarehe 1 Septemba 2022, nilichagua kupiga hadithi hapa kwenye IG pekee...sawa, je, hilo halipaswi kubadilika sasa tarehe 1 Septemba 2023? Likizo inaisha. Inapakia...” Maribe alisema.

Maribe, ambaye wakati mmoja alikuwa mwanahabari maarufu wa kisiasa na mtangazaji maarufu katika Royal Media Services, aligonga vichwa vya habari baada ya yeye na aliyekuwa mpenzi wake Joseph Irungu almaarufu Jowie kushtakiwa kwa kumuua mfanyabiashara Monica Kimani mwaka wa 2018.

Kesi hiyo ilisababisha mambo mengi ambayo yalimuathiri Maribe ikiwa ni pamoja na kuondoka katika runinga wakati kesi yake imekuwa ikiendea mpaka sasa.

Jaji Idris Nzioka aliyeketi katika Mahakama ya Sheria ya Milimani katika uamuzi wa Machi, alisema kwamba Maribe na Jowie wana kesi ya kujibu.

Maribe hakufichua angejiunga na jumba gani la media au ni aina gani ya kipindi angeandaa, lakini mashabiki wake walifurahi kumuona tena kwenye skrini.

“Karibu tena malkia,” mchekeshaji DJ Shit alisema.

“Kurudi daima kuna nguvu zaidi kuliko vikwazo,” mwingine alisema.

“Bado nina matumaini makubwa na kurudi kwako... Go gal 🔥🔥🔥” Mantashaa.

“Tumekukumbuka jackie hope unaendelea vyema” Nyambura Sophie.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved