logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kutana na mtangazaji wa Citizen TV aliyemtongoza HR miezi michache baada ya kuajiriwa

Mtangazaji huyo alisema kwamba mke wake wa sasa kipindi hicho alikuwa akifanya kazi kama HR.

image
na Davis Ojiambo

Burudani06 September 2023 - 09:12

Muhtasari


  • • Mtangazaji huyo alisema kuwa haoni kama kuna ubaya kwa mtu kuchumbiana na mfanyikazi mwenzake mradi mapenzi yenu hayaathiri utendaji wenu wa kazi.
Wycliff Orandi

Wycliff Orandi, mtangazaji wa runinga ya Citizen amefunguka jinsi alimpaka mkewe.

Katika mahojiano ya kipekee na Citizen Digital, Orandi aliwashangaza wengi alipofichua kwamba alikutana na mpenzi wake kazini.

Mtangazaji huyo alisema kwamba mke wake wa sasa kipindi hicho alikuwa akifanya kazi kama HR na hapo ndipo walijuana na baadae akamuomba kuwa mpenzi wake.

Orandi alisema kwamba yeye si mtu ambaye anaogopa kuzungumza na watu wa kitengo cha HR ambao mara nyingi huogopewa sana na wafanyikazi kwani wao ndio husimamia kitengo hicho cha kuajiri na kufuta.

“Tulipatana hapa kazini, alikuwa anafanya kazi kama HR na tulijuana… sielewi mbona watu wanaogopa HR, mimi siamini hilo. Kama wewe ni mtu mzuri na watu wanakukubali sidhani kama kuna haja ya kuogopa HR,” Orandi alisema.

Mtangazaji huyo alisema kuwa haoni kama kuna ubaya kwa mtu kuchumbiana na mfanyikazi mwenzake mradi mapenzi yenu hayaathiri utendaji wenu wa kazi.

“Mimi sioni kama kuna ubaya kwa watu kuchumbiana wakifanya kazi pamoja, mradi haiathiri kazi yenu kila mtu akae katika kitengo chao mkutane baada ya kazi. Kama nyinyi ni watu wamekomaa mtaelewana tu, mnaketi chini na kuwa na maelewano,” alisema.

Orandi si mtu pekee kuoana na mfanyikazi mwenzake katika kampuni ya Royal Media.

Itakumbukwa wanahabari Rashid Abdallah na Lulu Hassan ni wanandoa ambapo pia sadfa imewakutanisha katika zamu moja ya kufanya utangazaji wa habari na vipindi vya Kiswahili katika runinga ya Citizen.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved