Marioo adaiwa kutoa mahari ya shilingi milioni 5.8 za Kenya kumuoa Paula wa Kajala

Wiki jana, Marioo aliandika mitandaoni kwamba hakuwa tayari kuoa lakini kwa jinsi Paula anavyomchanganya kwa mapenzi, anatathmini kutibua mipango yake na badala yake kumuoa.

Muhtasari

• “Tayari ametoa mahari milioni 100,” Paula alijibu swali hilo huku wakicheka na mama yake na kujaribu kuficha nyuso.

Marioo akiwa na muhibu wake Paula.
Marioo akiwa na muhibu wake Paula.
Image: Instagram

Msanii wa kizazi kipya anayefanya vizuri kwenye muziki wa Amapiano wa Kibongo Marioo amedaiwa kutoa mahari ya shilingi milioni 100 za Kitanzania [Milioni 5.8 za Kenya] kwa ajili ya kumuoa bintiye mwigizaji Kajala Masanja, Paula Masanja.

Hili lilifichuliwa na Paula mwenyewe wakati wa mahojiano mafupi na mtu mmoja ambaye alikuwa anazungumza nyuma ya kamera.

Katika video hiyo, Paula na mamake Kajala walikuwa wamesimama huku wamekumbatiana wakati mtu huyo alimuulzia kuhusu maendeleo ya mahusiano yake na msanii Marioo.

Mtu huyo alimuuliza kama mahari tayari yametua ambapo binti huyo alijibu kwa tabasamu lenye haya kwamba tayari Marioo si mtu wa kupoa na ameshawasilisha mahari ya kiasi hicho cha pesa tayari kuitaka posa yake.

“Tayari ametoa mahari milioni 100,” Paula alijibu swali hilo huku wakicheka na mama yake na kujaribu kuficha nyuso.

Hata hivyo, jamaa huyo alionekana kutilia shaka kiasi hicho cha mahari akisema kwamba si kwa hela hizo ambazo Marioo anaweza kutumia kupata mkono wa Paula katika ndoa.

Paula baada ya kuthibitisha kuachana na Rayvanny miezi kadhaa iliyopita hakutulia na alirudi akijitangaza kuwa mpenzi wa Marioo.

Marioo naye amekuwa akitatradadi na mrembo huyo kilac sehemu katika penzi ambalo lilianza kama mchezo, wengi wakihisi wawili hao mwanzoni walikuwa pamoja kwa ajili ya kibiashara ambapo Paula alitarajiwa kuonekana kwenye muziki wa Marioo kama Vixen wa Video.

Wiki jana, Marioo aliandika mitandaoni kwamba hakuwa tayari kuoa lakini kwa jinsi Paula anavyomchanganya kwa mapenzi, anatathmini kutibua mipango yake na badala yake kumuoa Paula kabisa kama mke wake.