Kupumzika ni Mbinguni: Sidika atambulisha mpenzi mpya baada ya kuachana na Mauzo

Mwanasosholati huyo ambaye anakula bata marekani alionesha sura ya mwanamume mpya ikiwa ni wiki moja tu baada ya baba kwa wanawe wawili Brown Mauzo kuthibitisha wameachana.

Muhtasari

• "Maisha ni mafupi sana kujali jamii inafikiria nini. Nenda kafurahi nenda kapende nenda kaishi na ufurahie maisha. Maisha sio mtoto wa mazoezi." alisema.

• Hivi majuzi, Mauzo alifichua kuwa alikuwa akitafuta mchumba, huku akisisitiza kuwa yuko tayari kuendelea na maisha yake.

Vera Sidika na mpenzi mpya.
Vera Sidika na mpenzi mpya.
Image: Insta

Mwanasosholaiti Vera Sidika yuko kwenye vichwa vya habari kwa mara nyingine, safari hii akizungumziwa baada ya kumtambulisha yule anayekisiwa kuwa ni mwanaume aliyechukua nafasi ya Brown Mauzo katika maisha yake kama mpenzi.

Sidika ambaye yuko nchini Marekani na amekuwa akiwaonjesha mshabiki wake picha na video akila bata katika sehemu mbali mbali za taifa hilo lenye nguvu duniani alipakia picha ya mwanaume akiwa ameketi kwenye kochi na kuweka picha kubwa ya emoji ya mapenzi .

Mama huyo wa watoto wawili alishiriki picha ya mwanamume huyo lakini akamfunika kwa emoji ya mapenzi. Walakini kutokana na kile alichokionyesha, mwanamume huyo amejengeka vyema na ana nywele zilizosukwa rasta.

Sidika ambaye kwa mara nyingi watu humchukulia kama mtu wa kuigiza maisha aliambatanisha picha hiyo na kolabo ya Chris Brown na Nick Minaj – Do You Mind wala hakushiriki kitu kingine Zaidi cha kudokeza mapenzi Zaidi ya emoji.

Katika hadithi tofauti kwenye Instagram, alisema, "Maisha ni mafupi sana kujali jamii inafikiria nini. Nenda kafurahi nenda kapende nenda kaishi na ufurahie maisha. Maisha sio mtoto wa mazoezi."

Tetesi kuwa Vera amepata mapenzi tena ziliibuka baada ya kushiriki video akiwa ameshika mkono wa mtu asiyeeleweka. Wawili hao walikuwa wakielekea kwa kile kilichoonekana kuwa usiku wa kuamkia leo.

Maendeleo ya hivi punde yanakuja takriban wiki moja ambapo ex wa Vera, Browm Mauzo, alifichua kwamba hawakuhusika tena katika uhusiano wa kimapenzi.

“Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora sisi na watoto wetu kusonga mbele tofauti. Lengo letu sasa ni uponyaji na kukumbatia siku zijazo kwa mioyo iliyo wazi,” sehemu ya taarifa yake ilisoma.

Hivi majuzi, Mauzo alifichua kuwa alikuwa akitafuta mchumba, huku akisisitiza kuwa yuko tayari kuendelea na maisha yake baada ya kujivinjari na sosholaiti huyo kwa takribani miaka 3.

"Nataka rafiki bora ninayeweza kulala naye," alisema.

Pia amekuwa akishiriki nukuu za motisha tangu kutangaza kutengana kwao.