Mwanaume kufaulu maishani lazima uwe mchoyo kwa pesa zako - Akon, staa wa R&B

Akon mwenye utajiri wa dola milioni 60 ambacho ni kiasi sawa na shilingi za Kenya bilioni 8.8 alifichua kwamba duniani anadhani yeye ndiye mwanadamu mchoyo zaidi aliye hai.

Muhtasari

• Akon alifichua hili alipokuwa akishiriki kama mgeni katika kipindi kipya zaidi cha Impulsive Podcast.

• Kulingana na Akon, “Ikiwa unataka kubaki tajiri, kaa ubahili. Mimi ndiye mtu bahili zaidi duniani."

Akon
Akon
Image: Insta, Maktaba

Mwimbaji wa R&B kutoka Senegal na Marekani Akon ameshiriki ushauri wa kifedha kwa watu matajiri wanaotafuta kudumisha utajiri wao na kuepuka kupata pesa.

Msanii huyo alikuwa akitoa ushauri huu na pia kukiri kwamba hadhani kama kuna mtu au kutawahi tokea mtu duniani kote ambaye ni bahili kama yeye.

Akon alikiri wazi wazi kwamba yeye ndiye mtu mchoyo wa kutoa pesa Zaidi duniani.

Akon alisema mtu yeyote tajiri ambaye anataka kudumisha hali yake ya kifedha na kijamii inayovutia lazima avae vazi la ubinafsi.

Alifichua kuwa kuishi na kanuni iliyotajwa hapo juu kumemfanya aendelee kuwa tajiri, na kuongeza kuwa yeye ndiye "mtu mbaya zaidi duniani".

Alidai kwamba lazima iwe ubahili ili kudumisha hali yake ya utajiri.

Akon alifichua hili alipokuwa akishiriki kama mgeni katika kipindi kipya zaidi cha Impulsive Podcast.

Kulingana na Akon, “Ikiwa unataka kubaki tajiri, kaa ubahili. Mimi ndiye mtu bahili zaidi duniani."

Pia aliwashauri wafanyakazi wenzake na mashabiki kupinga kishawishi cha kumiliki ndege ya kibinafsi ikiwa wanataka "kusalia tajiri."

Msanii huyo ambaye ana usuli wa Senegal kulingana na jarida la Forbes mwezi Mei mwaka huu, utajiri wake wa jumla unasimamia dola milioni 60 ambacho ni kiasi sawa na shilingi za Kenya bilioni 8.8.

Je, ni kweli kwamba kwa mwanaume kufaulu maishani lazima awe bahili?