logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Zuchu ameweka wazi Diamond ndio mwanaume wa kwanza kulala naye na kumtoa ubikira

Diamond tayari ni baba kwa watoto wengi, akiwa na wawili na Zari, mmoja na Tanasha na mmoja na Hamisa Mobetto.

image
na Davis Ojiambo

Burudani10 September 2023 - 08:41

Muhtasari


  • • Kwa kile kilichooneaka kama ni kushangaza kwa wengi, Zuchu aliwataka watangazaji hao pia kumuuliza swali hilo Diamond.
  • • Diamond tena bila aibu alijibu kwamba hajawahi tembea na mwanamke mwingine kimapenzi Zaidi ya Zuchu tu.
Zuchu asema hawezi kumwacha Diamond

Msanii malkia wa Bongo Fleva Zuchu amethibitisha bayana kwamba bosi wake ambaye pia ndio mpenzi wake Diamond Platnumz ndoye mwanamume wa kwanza kushiriki kimapenzi.

Katika kile kiichoonekana kama ni kipindi cha maswali na majibu na mtangazaji wa Wasafi, walikuwa wamepewa vijikaratasi vilivyokunjwa na ambavyo ndani mwao kulikuwa kumeandikwa maswali kwa ajili yao kujibu.

Katika moja ya swali, Zuchu aliulizwa kujibu mpaka sasa ni wanaume wangapi ambao ameshatoka nao kimapenzi.

“Mpaka sasa ni wanaume au wanawake wangapi umeshawahi kulala nao kimapenzi,” swali liliuliza kwa mshangao wa Zuchu.

“Ni mmoja tu,” Zuchu alijibu huku akimkumbatia Diamond ambaye walikuwa wamesimama naye huku bosi huyo wa Wasafi akionekana kutojiweza kwa jinsi Zuchu alikuwa anampunga kwa mapenzi mubashara.

Kwa kile kilichooneaka kama ni kushangaza kwa wengi, Zuchu aliwataka watangazaji hao pia kumuuliza swali hilo Diamond.

Diamond tena bila aibu alijibu kwamba hajawahi tembea na mwanamke mwingine kimapenzi Zaidi ya Zuchu tu.

Diamond alijibu hili licha ya kujulikana wazi tena na kila mtu kwamba ameshatoka kimapenzi na wanawake wengi tena wenye hadhi za juu akiwemo Wema Sepetu, Hamisa Mobetto, Zari Hassan, Tanasha Dona na wengine baadhi tu kwa kutaja.

Zaidi ya hapo, Diamond tayari ni baba kwa watoto wengi, akiwa na wawili na Zari, mmoja na Tanasha na mmoja na Hamisa Mobetto.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved