Balaa: Ruger halisi wa Nigeria avunja kimya kuhusu Ruger feki kutoka Kayole Kenya

" Kusema kweli kwa njia Fulani anapromoti nyimbo zangu sababu unajua hajatengeneza ngoma zake akitumia jina langu bali anatumia ngoma zangu na jina langu,” alisema.

Muhtasari

• “Namtakia mema, nafahamu na ninafurahia kwa yale anayoyafanya. Anapiga mitikasi yake, kila mtu lazima ale,” Ruger alisema.

Ruger wa Kayole
Ruger wa Kayole
Image: Instagram//Ruger wa Kayole.

Msanii wa kizazi kipya kutoka Nigeria, Ruger kwa mara ya kwanza amevunja kimya kuhusu msanii wa kenya anayetamba kwa jina na muonekano wake baada ya Mkenya huyo kuanikiwa kutumbuiza katika shoo moja na mashabiki wengi kumshangilia wakidhani ni Ruger halisi kutoka Nigeria.

Katika klipu moja ambayo imezuka mitandaoni, Ruger halisi alikuwa katika mahojiano na BBC 1Extra nchini Uingereza alipoulizwa kama anamfahamu msanii huyo wa Kenya anayeandaa shoo kwa jina na muonekano wake.

Wengi walidhani kwamba Ruger halisi angetema moto kwa Ruger feki lakini cha kushangaza ni kwamba Ruger alisema haoni kama kuna ubaya kwa msanii chipukizi kutumia nembo yake ya muonekano na hata kutumbuiza ngoma zake kwani hiyo ni moja ya njia nyingi tu za kueneza muziki wake kwa mashabiki.

“Namtakia mema, nafahamu na ninafurahia kwa yale anayoyafanya. Anapiga mitikasi yake, kila mtu lazima ale,” Ruger alisema.

Alikiri kwamba watu wake walishawahi kumuambia kuhusu msanii huyo chipukizi wa Kenya lakini hakuona ubaya wowote kwani hiyo ni njia moja pia ya kumtangaza kimuziki.

“Kwa sababu wakati watu wangu walikuwa wananiambia kuhusu msanii huyo, umeona anavyofanay, nilisema hapana lakini nilisema mwanamume pia anajaribu kufukuzia riziki na unajua. Kusema kweli kwa njia Fulani anapromoti nyimbo zangu sababu unajua hajatengeneza ngoma zake akitumia jina langu bali anatumia ngoma zangu na jina langu,” alisema.

“Mwisho wa siku watu watakwenda nyumbani kwao na kutiririsha nyimbo hizo na hicho ndicho kitu cha muhimu Zaidi kwangu. Naomba kila shabiki wangu kutulia hakuna ubaya umetendwa,” aliongeza kwa ujasiri wa kiume.

Ruger wa Kayole akinukuu klipu hiyo, alimshukuru Ruger wa Nigeria akisema kuwa huo ndio moyo wa kiume.

"Asante sana ndugu yangu 🙏. tusaidiane"

Tazama video hii hapa akijieleza;