Video ya Rich Mavoko akitumbuiza mavumbini peku peku yawaliza mashabiki

Baadhi ya mashabiki walionekana wakijongea karibu naye na kumpa vijisenti vya kufutia jasho. Wengine walimlaumu Diamond kwa kumsaini Wasafi waksiema huo ndio ulikuwa mwanzo wa kupotea kwake kimuziki.

Muhtasari

• Lakini baada ya kuingia Wasafi, msanii huyo alifana na kunawiri kwa muda mfupi kabla ya kushindwa tena kuendelea na akaishia kutoka kimya kimya.

• Baadhi ya mashabiki walioguswa na utumbizaji wake walionekana wakijongea karibu naye na kumpa vijisenti vya kufutia jasho.

Rich Mavoko
Rich Mavoko
Image: Instagram,TikTok

Siu chache zilziopita kuliibuka na video katika mitandao ya kijamii zikimuonesha msanii Rich Mavoko akiwa katika hali ya kutamausha ambapo alikuwa anatumbuiza mbele ya umati mdogo tena kwenye mchanga wa vumbi akiwa peku.

Video hiyo ilizua maoni changamano kutoka kwa mashabiki wa msanii huyo ambaye alikuwa na taaluma angavu kabla ya kusainiwa katika lebo ya Wasafi na kufulia kabla ya kuondoka.

Mavoko katika mapema miaka ya 2013 hadi 2018 alikuwa ni mmoja kati ya wasanii ambao walikuwa wanapigiwa upato mkubwa kumpa ushindano wa aina yake Diamond Platnumz kwa jinsi alikuja na mihemko kwa kuachia vibao moto kama vile Pacha Wangu, Moyo Wangu, miongoni mwa vingine.

Lakini baada ya kuingia Wasafi, msanii huyo alifana na kunawiri kwa muda mfupi kabla ya kushindwa tena kuendelea na akaishia kutoka kimya kimya.

Baada ya kutoka, alijitahidi kufanya kazi za muziki kwa kujisimamia japo muda si kitambo aliingia gizani asionekane tena, huku kila akitoa wimbo hauendi mbali na hatimaye kusahaulika na mashabiki waliokuwa wanampenda.

Baadhi ya mashabiki walioguswa na utumbizaji wake walionekana wakijongea karibu naye na kumpa vijisenti vya kufutia jasho.

Sasa baada ya hivi majuzi video hiyo kuibuka, mashabiki walitoa maoni kinzani baadhi wakionesha kuchukizwa na kile walisema kuwa asingeingia Wasafi mpaka sasa hivi pengine angekuwa hajafulia katika taaluma yake.

Mavoko alikuwa anajitahidi kuwatumbuizia mashabiki wachache katika uwanja wa tambarare kwa kunengua lakini maskini wa Mungu alionekana kuwa mnyonge sana.

Haya hapa ni baadhi ya maoni ya mashabiki walioonekana kwa kiasi kikubwa kumtupia lawama aliyekuwa bosi wake Diamond kwa kile walisema alimtoa kwenye ramani ya njia kuu kwa kumsaini na baadae kumuingiza kwenye chaka.

“Rich Mavoko angebaki Kaka empire kutoka kitambo...🤔Diamond alimharibu,” Rouzey alisema.

“siamini haya mbona mavoko,” mwingine alisema.

“Nilichokipenda kwake ni ule msemo,mtaftaji hachoki,wala mazingira hayamsumbui..as long he’s fighting for himself,who are we to judge?? Tuunge mkono” Mwanza Salon alisema.

“huyu jamaa alikuwa same level na diamond platnumz what happened?” Ni Jwa Tsana aliuliza.

Maoni yako ni yepi?