Eric Omdondi na wengine 17 kulipa faini ya elfu 10 au mwezi mmoja korokoroni

Haya yanajiri baada ya miezi nane tangu wakati Eric na wenzake kufanya maandamano nje ya Bunge.

Muhtasari

•Kwenywe kesi hiyo, Omondi na wenzake walioshiriki katika maandamano hayo walitakiwa kuhudumia kifungu cha mwezi mmoja korokoroni au kulipa  shilingi elfu 10 kila mmoja 

•Eric na wezanke, walikiri mbele ya Jaji wa mahakama ya hakimu ya milimani kuwa na hatia

Eric Omondi akiwa mahakamani
DOUGLAS OKIDY Eric Omondi akiwa mahakamani
Image: Mchekeshaji Eric Omondi

Mwigizaji Eric Omondi pamoja na wenzake 17 wamesomewa hukumu ya mashtaka yao. 

Hii ni baada ya kesi iliyowasilishwa mahakamani ya kuwashitaki kwa kufanya maandamano nje ya bunge la kitaifa kuskilizwa na kusomwa na Jaji Lukas Onyina , wa mahakama ya hakimu Milimani hapa mjini Nairobi, Septemba 15.

Eric na wezanke, walikiri mbele ya Jaji wa mahakama ya hakimu ya milimani kuwa na hatia.

Kwenywe kesi hiyo, Omondi na wenzake walioshiriki katika maandamano hayo walitakiwa kuhudumia kifungu cha mwezi mmoja korokoroni au kulipa  shilingi elfu 10 kila mmoja ambazo Jaji Onyina alizitaja kuwa faini,

"Dhaman ya pesa taslimu itachukuliwa kuwa faini."

Mnamo Februari 21,2023, Eric Omondi akiwa na kikundi cha mashabiki ambao wanakisiwa kuwa walinzi wake, walijitokeza na kufanya maandamano nje ya jengo la bunge la Kitaifa.

Maafisa wa polisi walifika kwa haraka  na kuwasambaratisha  huku Omondi na wenzake 17 kukamatwa.

Polisi walidai kuwa bunge la kitaifa ni jumba ambalo hujiususha na mjadala wa mambo yanahuyu Taifa na hivy halitakiwi kuwa na usumbufu wowote.

Eric kwa upande wake, alidai walikua na lengo la kumuona Spika wa bunge ili kumkabidhi malalamishi na maslahi ya wakenga ambao alieleza kuwa wanakumbwa na hali ngumu ya maisha.

Hata hivyo Eric amekuwa akijishirikisha kwa shughuli ambazo kwa madai yake ni za kuwatetea Wakenya ambao anasema wameshindwa kukabiliana na hali ngumu ya maisha.