Mwanawe rais wa USA, Joe Biden aonekana akipanga foleni kupatiwa pizza ya bure

Akiwa na mke wake Melissa Cohen na mwanawe Beau, Hunter alifika kwenye sherehe ya kuzindua Burgers ya Irv na Prince Street Pizza karibu na makazi yake ya Malibu.

Muhtasari

• Muda mfupi baada ya kupokea mlo wake nzuri, Hunter alisimamishwa na mtu asiyejulikana kwa mazungumzo mafupi kabla ya kurudi kwenye SUV nyeusi.

Mwanawe Joe Biden, Hunter Biden.
Mwanawe Joe Biden, Hunter Biden.
Image: X

Mtoto wa kwanza wa rais wa Marekani Joe Biden, Hunter Biden ambaye anakabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya bunduki alionekana amepanga foleni kupokea pizza ya bila malipo, saa chache kabla ya kufunguliwa mashtaka hayo.

Kwa mujibu wa picha zilizovujishwa mitandaoni nchini Marekani, Hunter alionekana akipokea pizza akiwa amemshikilia mwanawe mkononi saa chache kabla ya waendesha mashtaka wa serikali kumfungulia mashtaka huko Delaware kwa mashtaka yanayohusiana na kijana huyo wa miaka 53 kusema uwongo kuhusu uraibu wa dawa za kulevya aina ya crack wakati alinunua bunduki mwaka wa 2018.

Akiwa na mke wake Melissa Cohen na mwanawe Beau, Hunter alifika kwenye sherehe ya kuzindua Burgers ya Irv na Prince Street Pizza karibu na makazi yake ya Malibu, Calif.

Muda mfupi baada ya kupokea mlo wake nzuri, Hunter alisimamishwa na mtu asiyejulikana kwa mazungumzo mafupi kabla ya kurudi kwenye SUV nyeusi, iliyoambatana na walinzi wake wa kisiri.

Hunter anashutumiwa na wakili maalum David Weiss kwa kusema uwongo kuhusu matumizi yake ya dawa za kulevya kwenye fomu ya kununua bunduki mwaka wa 2018, aliponunua bastola ya Colt Cobra katika kipindi ambacho alikuwa akitumia vibaya mihadarati - kama alivyokiri katika risala yake ya 2021 "Beautiful Things.”

Bunduki hiyo ilitupwa kwenye pipa la takataka nyuma ya duka la chakula mnamo Oktoba 23, 2018, na binti-mkwe wa kwanza Hallie Biden, ambaye aliolewa na kaka ya Hunter, Beau, hadi kifo chake mnamo 2015 na kisha kuchumbiana na Hunter.

Mashtaka hayo yana adhabu ya juu zaidi ya miaka 25 jela na Hunter anaweza kukabiliwa na kesi za ziada za uhalifu huko DC na Los Angeles kwa ulaghai wa kodi na ushawishi haramu wa kigeni, miongoni mwa makosa mengine yanayowezekana.