Mwili wa aliyekuwa mwanahabari wa Capital FM, Sean Cardovillis wachomwa

Kufuatia tukio hilo, familia yake imetangaza kuwa ibada ya kumbukumbu itaandaliwa Ijumaa wiki ijayo katika Kanisa Katoliki la Consolata Shrine huko Westlands, Nairobi.

Muhtasari

• Rais William Ruto na naibu wake Rigathi Gachagua waliongoza nchi kumsifu mwanahabari huyo, wakimkumbuka kwa "ustadi na ari yake" katika tasnia ya habari.

Sean Cardovillis
Image: Facebook

Siku sita tu baada ya kifo cha mwanahabari wa michezo wa stesheni ya Capital FM, Sean Cardovillis, maiti yake imeripitiwa kuteketezwa katika makaburi ya Kariakor jijini Nairobi.

Cardovillis ambaye amekuwa kweye tasnia ya uanahabari wa runinga ya redio humu nchini kwa muda mrefu aliripotiwa kufariki mapema Jumamosi asubuhi katika makazi yake Westlands, Nairobi.

Cardovillis alichomwa katika sehemu ya kuchoma maiti za raia Wahindi kama ilivyo desturi yao.

Kufuatia tukio hilo, familia yake imetangaza kuwa ibada ya kumbukumbu itaandaliwa Ijumaa wiki ijayo katika Kanisa Katoliki la Consolata Shrine huko Westlands, Nairobi.

Wakati wa kufariki kwake, Cardovillis alikuwa mtangazaji wa habari za michezo katika Capital FM, akiwa na taaluma yake iliyochukua miongo kadhaa.

Ingawa mwajiri wake hakutoa maelezo kuhusu ugonjwa wake, walibainisha kuwa kwa miaka minne iliyopita, Sean alikuwa akisumbuliwa na afya mbaya, na alikuwa akiingia na kutoka hospitali.

Rais William Ruto na naibu wake Rigathi Gachagua waliongoza nchi kumsifu mwanahabari huyo, wakimkumbuka kwa "ustadi na ari yake" katika tasnia ya habari.

Alipangiwa kufanya mahojiano na bingwa kadhaa wa dunia na Olimpiki na mshikilizi wa rekodi ya dunia mara tatu Faith Kipyegon kabla ya kifo cha ghafla.

 

Alikuwa na shauku ya motocross. Mnamo Juni 2023 alirejea Capital FM baada ya miaka 18.