• Alianza kwa kumtambulisha kwa jina lake la kimajazi, Zari The Bosslady na kwenda mbele kummiminia sifa kwa maneno matamu.
Mumewe Zari Hassan, Shakib Cham Lutaaya ameonekana kwenye video akimsifia mjasiriamali huyo kwa maneno na majina matamu.
Katika video hiyo, wapenzi hao walikuwa wameketi nje mbele ya nyumba yao na Shakib ndiye alikuwa na simu akirekodi video hiyo huku Zari akiwa ameketi kando yake.
Alianza kwa kumtambulisha kwa jina lake la kimajazi, Zari The Bosslady na kwenda mbele kummiminia sifa kwa maneno matamu.
Alimtaja kama rais wa mitaani, msemaji wa ghetto, mashine ya ATM inayotema pesa mpya mpya miongoni mwa sifa nyingine tumbi nzima.
“Zari the Bosslady, rais wa mitaani, balozi wa ghetto, sauti ya pesa, mtu bora Zaidi wa Afrika Mashariki,” Shakib Lutaaya alisema huku Zari akishindwa kuzuia tabasamu lake.
“Kamanda wa mstari wa mbele vitani, Mashine ya ATM, kopi ya asili, kakangu kutoka kwa mama mwingine, superman wa kingkong… ndio wewe ni superman wa kingkong,” Shakib aliongeza.
Video hiyo inaibuka ikiwa ni miezi michache tu baada ya uvumi kuibuka kwamba uhusiano wao ulikuwa umegonga mwamba wa bahari kufuatia sauti iliyokisiwa kuwa ya Zari akimzungumzia kwa njia ya kebehi mpenzi huyo wake.
Sauti ambayo ilivujishwa na Mtanzania mmoja ilisikika mtu kama Zari akimtaja Shakib kama mtu mwoga asiye na mwelekeo wa maisha kitu ambacho kilitajwa kuwa kilimkasirisha sana Shakib.
Kijana huyo ambaye ni mdogo kiumri kwa Zari aliandika ujumbe wa kutaka kuheshimiwa mitandaoni lakini hawakutajana moja kwa moja.