Ndoto yangu ilikuwa kuwa wakili-Samidoh afichua

Kama angekuwa wakili, Samidoh angekuwa katika uwanja huo na mama wa watoto wake Karen Nyamu

Muhtasari
  • Akionyesha sehemu ya matokeo yake ya KCPE, Samidoh alikariri kwamba ndoto yake ya kuwa wakili ingali halali
Samidoh katika sare ya polisi
Image: HISANI

Msanii wa Mugithi Samidoh ameelezea na kufichua ndoto yake ambayo alikuwa anatazamia kuwa.

Kulingana na baba huyo wa watoto watano, alitaka kuwa wakili.

Kinyume na matarajio yake Samidoh aliendelea kuwa Afisa wa Polisi na mwimbaji

Ni miongoni mwa wasanii maarufu wa Mugithi nchini Kenya.

Akionyesha sehemu ya matokeo yake ya KCPE, Samidoh alikariri kwamba ndoto yake ya kuwa wakili ingali halali

Kulingana na matokeo alikuwa Index 1.

"Hiyo index number one wa kwenu anafanyanga nini siku hiziI aspired to be a lawyer.Saa hii mimi ni One man guitor AKA. Singing police man Dreams not shattered bado nakula mbuku."

 

Meneja wake Moses Marite pia alishiriki matokeo yake akisema alikuwa index 1.

"Wale wanauliza Samidoh alipata ngapi kwa hesabu, alikuwa Index 001 mimi Index 005...All I ever dreamed was to become an engineer , sasa mimi ni memeer(memer)

Kama angekuwa wakili, Samidoh angekuwa katika uwanja huo na mama wa watoto wake Karen Nyamu

 

 

 

 

 

Samidoh katika sare ya polisi
Image: HISANI