Harmonize alikuwa anaandikiwa ngoma za Kiingereza na CountryBoy - H Baba adai

“Mimi nakwambia mdogo wangu [Harmonize] kama una uhakika una hati ya nyumba, ita waandishi wa habari mimi nakuja kama sijavaa nguo,” H Baba alimwambia Harmonize.

Muhtasari

• Kando na kudai kwamba Country Boy ndiye alikuwa anaandika ngoma za Kiingereza kwa ajili ya Harmonize, H Baba pia alidai mavazi alikuwa anafunzwa na Country Boy.

H Baba na Harmonize
H Baba na Harmonize
Image: insta

Takribani miaka miwili tangu msanii Country Boy kuondoka katika lebo ya Konde Music Worldwide inayomilikiwa na Harmonize, msanii mkongwe H Baba amekiri kwamba yeye ndiye aliyemshawishi kuondoka katika lebo hiyo.

H Baba ambaye alikuwa anazungumza na waandishi wa habari za mitandaoni kwa majigambo alisema kwamba alimshawishi Country Boy kuondoka KOnde kutokana na kile alisema kwamba wasanii hao walikuwa wanafanya kazi kubwa lakini wakati wa mafanikio Harmonize anadai wazi wazi kwamba mafanikio yamechangiwa na wanawake aliokuwa anachumbiana nao.

H Baba alidai kwamba Harmonize hakuwa anqajua lolote hata ngoma za lugha ya Kiingereza alikuwa anaandikiwa na Country Boy, pamoja pia na kufunzwa jinsi ya kuvaa mavazi ya kupendeza.

“Watu wameweka mzigo kwa wale wasanii, wewe hujawapa wasanii ule mzigo wao. Wale wasanii umevunja mkataba na wao, wanaondoka Ziiki inaenda kumdai nani? Mimi niseme tu ukweli mimi ndio nimemtoa Country Boy pale [Konde Gang],” akasema H Baba.

“Ngoma alikuwa anaandikiwa na Country Boy kwa lugha ya kiingereza. Kuvaa alikuwa anafunzwa na Country Boy, vaa hivi, kaa hivi toka hivi, si unajua tena kinyamwezi, Country si mnamjua. Sasa siku tunaenda kuchukua tuzo pale, anafika anasema ‘ahsante Kajala’” H Baba aliongeza.

Alimpa changamoto Harmonize akisema kwamba ikiwa Harmonize ana hati ya nyumba basi yuko radhi kuita mkutano na vyombo vya habari na yeye – H Baba – atafika pale akiwa bila nguo.

“Mimi nakwambia mdogo wangu [Harmonize] kama una uhakika una hati ya nyumba, ita waandishi wa habari mimi nakuja kama sijavaa nguo,” H Baba alimwambia Harmonize.