Sina muda wa Ex wangu mimi-nikishaacha nimeacha asema Lady Jaydee

Mimi nikishaachana na mtu tunaachana,maana kama mwanzo hakuwa mzuri anawezaje kuwa mzuri

Muhtasari

•Jaydee anasema yeye ikitokea wameachana na mwanaume basi yeye hawezi akamrudia,akisema kuwa mkiachana mnaachana tu na kila mtu anaendelea na mambo yake

Lady Jaydee/Instagram
Lady Jaydee/Instagram

Mwanamuziki Judith Wambura  Mbimbo,maarufu Lady Jaydee wa Tanzania amesema hana kinyongo na mchumba wake wa zamani.

Jaydee anasema yeye ikiwachana na mwanaume hawezi akamrudia,akisema kuwa mkiachana mnaachana tu na kila mtu anaendelea na mambo yake .

Amesema kwamba kuachana haimanishi kuwa hamtapatana na kula au kunywa pamoja naye. Alisema mnaweza kusalia marafiki naye ila sio swala la mahusiano.

Cha kushangaza ni kwamba anasema kuwa anaweza kumuunganishia ex wake kupata mke,akijitofautisha na wanawake wengine ambao wana bifu rohoni au kuwa na bifu na ex wake.

Kwenye jumbe za Instagram alisema; 

"Mimi nikishaachana na mtu tunaachana, maana kama mwanzo hakuwa mzuri anawezaje kuwa mzuri,sina bifu m."

Aliendelea kusema kwenye video hiyo aliyoshiriki akisema kuwa kuachana si mwisho wa mawasiliano.

"Unajua kuachana sio ugomvi, mnaweza mkawa marafiki ila mafikirio ya kuwa mkiwa na ex wako hivyo mumesharudiana ndio hayafai.'

Mwimbaji huyo anasema kuwa ni vyema baada ya kuachana unapata uzoevu wa hali mpya angalau ya kusimulia kwa marafiki jinsi hali ilivyo.

Aansema anaweza kumpa ex wake ushauri na hata kumtafutia mchumba manake anachotaka ni uhusiano mwema ili kuendelea kuishi bila mawazo.

Lady Jaydee alichaguliwa kuwa Msanii Bora wa Kike wa R&B wa Tanzania mwaka 2002, alitumbuiza kwenye Shindano la Kora All Africa Designers, na alipata tuzo la "Albamu Bora ya R&B" katika Tuzo za Muziki Tanzania tarehe 6 Agosti 2004.

Julai 2005, alishinda tuzo ya "bora." video ya kike ya Afrika Kusini". Alikuwa miongoni mwa wanawake wa kwanza kuimba R&B kwa Kiswahili.

 Pia anajulikana kama Malkia wa Bongo Flava (Muziki wa Tanzania).