logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Embarambamba avunja kimya kuhusu wimbo unaozua mkanganyiko mitandaoni 'Mungu Ninyonye'

Pia alitetea hatua yake ya kuvaa mavazi ya kike.

image
na Davis Ojiambo

Burudani27 September 2023 - 08:16

Muhtasari


  • • Hata hivyo, msanii huyo alitetea hatua ya kutumia maneno kama hayo ambayo yanachukuliwa na kizazi cha sasa nje ya muktadha.
Embarambamba akuja na wimbo mpya.

Msanii wa injili ambaye pia ni mchekeshaji kutoka Kisii, Chris Embarambamba hatimaye amevunja kimya kuhusu wimbo wake mpya wa injili – Mungu Ninyonye – ambao umezua mkanganyiko na mtafaruku mitandaoni siku chache baada ya kuachilia wimbo huo.

Akizungumza katika chaneli ya 2Mbili TV, Embarambamba alianza kwa kuweka msimamo wake kuhusu wimbo huo, akisisitiza kwamba ni wa injili lakini akawalaumu Wakenya na watumizi wa mitandao ya kijamii kwa kuwa na akili potovu.

Msanii huyo alisema kwamba mstari anaomtaka Mungu Kumnyonya hakuwa anamaanisha kile ambacho watu walifikiria bali lengo lake lilikuwa ni Mungu kumfyonza dhambi zote kutoka kila sehemu ya mwili wake.

“Mimi nilikuwa namwambia Mungu sijui uko pande gani, ukiwa mbele ukiwa nyumba au pande zote ninyonye dhambi zangu ili nipate nguvu, nisukume maisha na niendelee kukutumikia. Lakini sasa wananchi, eehee… walikuwa wanahariri na kukata pale penye nimeimba ‘ninyonye’ wanaweka mitandaoni mpaka hata wewe ukiangalia unajiuliza hii ni injili kweli?” Embarambamba alisema.

Hata hivyo, msanii huyo alitetea hatua ya kutumia maneno kama hayo ambayo yanachukuliwa na kizazi cha sasa nje ya muktadha.

“Wimbo unatakiwa kusema ‘nataka Mungu nitoe dhambi zangu’ lakini kuna maneno ambayo unapata yamekuwa ya kuzoeleka eti ‘toa dhambi, sijui nini’ sasa nikaona hii kunyonya halijakuwa la kuzoeleka kwa watu. Natumia maneno ‘ninyonye dhambi zangu’ kuliko kusema nitoe dhambi zangu kwa sababu kutoa dhambi Mungu hawezi kuangalia hicho ni kitu kipi kwa sababu kuna wengi ambao wameimba hivyo,” alieleza.

Kando na wimbo huo ambao ulizua gumzo mitandaoni, msanii huyo mwenye mazoea ya kuvaa mavazi ya kike alieleza mbona anafanya hivyo licha ya kwamba pia alikiri wazi kujua Biblia kukataza wanaume kuvaa mavazi ya kike.

“Unajua kuna mahali Biblia inasema mwanamume asivae mavazi ya wanawake. Hiyo ni kitambo, tuelewane. Huu muziki tuko nao sasa hivi Wakenya ni lazima tutafute pesa kwanza tuweke hapa [tumboni] ndio tupate nguvu ya kufanya kazi ya Mungu,” alitetea hatua yake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved