Nasemwa sana na nilikua natarajia hayo- Bill Nass

Bill Nass amewajibu wanaomsema mitandaoni kuhusu video ya wimbo wa mkewe aliyoifanya.

Muhtasari

•Rapa huyo alijibu kuhusu video ambayo imesambaa mitandaoni akicheza wimbo wa mke wake Nandy unaojulikana kama `FLOW`.

• Amewaomba watu wanomsema kuelewa kwamba ni njia moja ya kuonyesha upendo kwa umpendao na kumuonyesha kuwa unamsapoti.

Bill Nass/Instagram
Bill Nass/Instagram

Msanii  Nicholaus Lyimo kutokea Dar es Salaam, Tanzania almaarufu, Bill Nass amewajibu wanaomsema mitandaoni kuhusu video ya wimbo wa mkewe aliyoifanya.

Rapa huyo alijibu kuhusu video ambayo imesambaa mitandaoni akicheza wimbo wa mke wake Nandy unaojulikana kama `FLOW`.

Hii ni baada ya msanii Mooh Savage,kumuuliza ilikuwaje akafanya video ya wimbo huo, na anajiskia aje kuona watu wakisema sana kuhusu yeye kucheza wimbo huo.

Kwenye mahojiano na shirika za burudani nchini Tanzania, Bill Nass alisema kwamba alikua anatarajia hilo;

"Nasemwa sana lakini niliyatarajia hayo." Alisema.

Alieleza kuwa alicheza wimbo huo na nia ya kumsapoti mke wake na kumuonyesha upendo alionao kwake.

"Mimi kwa nafsi yangu, sio clip nlikuwa nataka kuifanya, lakini kwa namna ambavyo nampenda mke wangu,ilibidi nivunje miiko yangu. Nilikuwa nataka kumsapoti kwenye mambo yake.

Hivyo amewaomba watu wanomsema kuelewa kwamba ni njia moja ya kuonyesha upendo kwa umpendao na kumuonyesha kuwa unamsapoti.

Hata ivyo amedokeza kuwa wakati mwingine upendo unaweza ukafanya mambo ambayo haukukusudia.

Bill Nass ni mume wa Mwanamuziki maarufu Nandy. Wawili hao walianza kuchumbiana mwaka wa 2020.

Walipata kuoana mwaka wa 2022, na wamebarikiwa na mtoto mmoja. Wote wanajishughulisha na tasnia ya muziki ambao ni maarufu sana Afrikan hasa Afrika Mashariki.

Japo anasema hakudhamiria kufanya video hiyo,ila anasema bado iko na wanaosema waseme tu bora mkewe yuko sawa nayo.