Kamene Goro Azungumzia tuhuma za Kulala na Obinna na Kibe

Kamene alipuuzilia mbali madai hayo na kuyaona kuwa ya uvumi tu akisema walikuwa marafiki tu na Oga Obinna na Andrew Kibe

Muhtasari

• Mtangazaji huyo wan zamani ambaye alikuwa akihojiwa kwenye Tuko Extra, aliangazia kuwa madai hayo yalikuwa mengi.

Kamene Goro/Instagramu
Kamene Goro/Instagramu

Aliyekuwa mtangazaji Kamene Gor, amejitokeza wazi kuhusu tetesi kuwa aliwahi kushiriki tendo la kimapenzi na Oga Obinna na Andrew Kibe.

Kamene ambaye alikuwa akihojiwa kwenye Tuko Extra, aliangazia kuwa madai hayo yalikuwa mengi.

Akisema kuwa yalianza na Andrew Kibe ambaye alifanya kazi naye awali katika redio ya NRG na baadaye Jalang’o alipoingia kufanya kazi katika Kiss 100.

Kamene alipuuzilia mbali madai hayo na kuyataja kama tu uvumi akisema walikuwa marafiki tu na Oga Obinna na Andrew Kibe.

Alidokeza kwamba uvumi huo ulikuwa labda kwa sababu alikuwa na marafiki wengi wa kiume kulinganisha na wa kike.

“Ilianza nikiwa nafanya kazi na Kibe, ikawa nilikuwa na Jalango halafu sasa ikawa Obinna. Kwa kweli nina marafiki wengi wa kiume kuliko marafiki wa kike. Tuna urafiki mzuri sana. Nimemfahamu Obinna kwa muda mrefu kwa njia ile ile niliyomjua Jalang’o kwa muda mrefu sana. Sisi ni marafiki tu, yaani haijawahi pita  chochote zaidi ya hapo,” Alisema.

Alipoulizwa kuhusu jinsi mumewe DJ Bonez alihisi kuhusu madai hayo, Kamene alishikilia kuwa ilimbidi kumwendea mumewe waziwazi na kwamba hakuwa na shaka na jambo hilo.

Aidha alisema kuwa ndoa yake na DJ Bonez inatokana na uaminifu kwa hivyo hakuna siri kati yao.

"Nilikutana na Bonez mara ya kwanza nikiwa na miaka 24. Nilikuwa nikirudi Kenya. Hatukupendana hata kidogo na nadhani nilisikia mengi juu yake na aliponifahamu aligundua jinsi watu walivyokosea. Alikuwa  maoni yake mwenyewe juu yangu. Yeye sio mtu anayeweza kunishuku tu nje ya mahali pa kwanza kwa sababu muda mwingi tunakuwa pamoja.” Aliongeza.