Minne asema yuko tayari kumaliza ugomvi na Ntalami ila kwa Masharti

Ugomvi kati ya wawili hawa ulianzia kwenye uundaji wa kikundi cha maudhui ya Real Housewives of Nairobi Msimu wa kwanza.

Muhtasari

• Minne ameeleza kuwa yuko tayari kutafuta njia mbadala za kusuluhisha tofuati zao,mradi tu Ntalami amuombe msamaha hadharani.

• Katika madai yake,Minne anataka kulipwa fidia ya sh 3 milioni kutoka kwa Ntalami kwa madai ya kuchafua chapa na sifa yake kwenye mitandao ya kijamii kupitia kile anachoeleza kuwa kesi ya uwongo dhidi yake.

Michelle Ntalami na Minne.
Michelle Ntalami na Minne.
Image: Insta

Mshiriki wa kundi la Real Housewives wa Nairobi Minne Kariuki,amesema yuko tyari usuluhisha zozo unaoendelea kati yake na mwanaharakati wa mitando y jamii Michelle Ntalami nje ya mahakama ila kwa sharti.

Minne ameeleza kuwa yuko tayari kutafuta njia mbadala za kusuluhisha tofuati zao,mradi tu Ntalami amuombe msamaha hadharani.

Ugomvi kati ya wawili hawa ulianzia kwenye uundaji wa kikundi cha maudhui ya Real Housewives wa Nairobi Msimu wa kwanza.

Mapema wiki hii Ntalami alianzisha hatua za kisheria dhidi ya Minne pamoja na shirika la uzalishaji la RHON,akimtuhumu Minne kwa kumchafulia jina. Katika kujibu Minne alifungua kesi dhidi ya Ntalami kwa kashfa.

Katika madai yake,Minne anataka kulipwa fidia ya sh 3 milioni kutoka kwa Ntalami kwa madai ya kuchafua chapa na sifa yake kwenye mitandao ya kijamii kupitia kile anachoeleza kuwa kesi ya uwongo dhidi yake.

Minne anasisitiza kuwa kesi ya Ntalami ni ya uwongo,kwa sababu bado hajmhudumia kwa nyaraka za shauri rasmi. ameendelea kusema kuwa kesi ya Ntalami ya uwongo kwenye mitandao imekuwa na athari mbaya kwa chapa yake.

Kwa sababu hizi Minne anadai faini iliyoanishwa ya milioni tatu. Yuko tayari kuendelea na madai haya mahakamani ikiwa Ntalami hatatimiza masharti yaliyoinishwa katika barua yake ya madai ikiwa ni pamoja na kuomba msamaha mbele ya umma.

Wakili wa Minne Peter Njage,alisisitiza kuwa mteja wake ni mshawishi na mtu maarufu ambayesifa yake ni muhimu kwa kazi yake. Alielez kuwa uenezaji wa Ntalami wa taarifa zilizodhibitiwa na zenye ni mbaya una uwezo wa kudhuru maish ya Minne.

Licha ya uaribiu huo uliofanyika,Njae alidokeza kuwa,wako tayari kutatua swala hilo kwa amani,bila kukimbilia mahakamani. Ila hili linategemea nia ya Ntalami kutimiza masharti y Minne.