Msanii Whozu akiri wazi wazi kwamba amewekwa na Wema Sepetu

Whozu aliimba sifa kochokocho kwa Wema SDepetu akimsifia kwa kumweka bila kumlipisha kodi ya nyumba.

Muhtasari

• Whozu alimuimbia Wema Sepetu na kusema kwamba yeye ndiye amemuweka nyumbani kwake na wala haoni aibu kusema hivyo.

Wema Sepetu ni mjamzito, Whozu afichua.
Wema Sepetu ni mjamzito, Whozu afichua.
Image: Instagram

Msanii ambaye pia ni muigizaji Whozu kutoka Tanzania amekiri wazi wazi kwamba anakaa kwa mpenzi wake ambaye pia ni muigizaji Wema Sepetu.

Whozu alifuchua haya akiwa jukwaani Iringa wakati wa tamasha linaloendelea la Wasafi.

Akiwa jukwaani, mashabiki walianza tambo za kumuimbia nyimbo wakitaja Wema Sepetu jambo lililomchochea pia kuimba naoi li kupandisha mzuka.

Whozu alimuimbia Wema Sepetu na kusema kwamba yeye ndiye amemuweka nyumbani kwake na wala haoni aibu kusema hivyo.

“Wema huyo, Weeema Wema nakaa kwake eeh, Wema Wema huyo Wema,” Whozu aliimba.

Penzi la Wema na Whozu limeduku kwa Zaidi ya mwaka mmoja huku katikati kukiwa na ukakasi kwamba huenda halitodumu.

Whozu amefichua haya siku chache tu baada ya video ikimuonesha mamake Wema akitimba katika hafla moja kwa fujo na kuonekana kumtuhumu binti yake kwa kuwa na mpenzi – Whozu- bila ya kumtambulisha kwake rasmi kama mpenzi wake.

Siku ya Alhamisi, wiki jana, Bi Mariam alipokuwa akitoa hotuba yake wakati wa karamu ya bintiye alimkosoa kuhusu uhusiano wake na mwimbaji Whozu akitaja kuwa haukubarikiwa.

Chapisho la Wema Sepetu la Alhamisi jioni linadokeza kuwa tukio la wiki iliyopita lilimuumiza sana muigizaji huyo na kumuacha na majeraha moyoni.

Wema katika mkutano na waandishi wa habari Jumapili jioni, aliahidi kwamba ifikapo Jumatatu saa nne usiku, ataweka wazi kila kitu katika mahojiano kwenye kituo kimoja cha redio, kile alichokisema kwamba ni ukakasi wote atakaoutoa.