Diamond na Nyashinski kutumbuiza mashabiki Nairobi katika Octobafest

Diamond anararajiwa kutubuiza wafuasi wake huku sherehe hizi zikileta pamoja wasanii wa Afrika Mashariki

Muhtasari

•Tamasha hili ni sherehe kubwa ya utamaduni wa Afrika Mashariki, inayoleta watu pamoja ili kufurahia ladha, sauti na tamaduni za kipekee za maeneo yote ya muziki wa Afrika.

Diamond Platnumzs
Image: Facebook

Mwanamuziki na nyota wa Bongo Tanzania Diamond Platnumz anatazamiwa kuwatumbuiza mashabiki wake mwishoni mwa mwezi katika uwanja wa Ngong Racecourse katika Oktobafest mjini Nairobi.

Tamasha ambalo linatarajiwa kuleta pamoja na kushirikisha nyota wa Kenya Nyashinski na John Frog wa Sudan Kusini.

Ann-Joy Michira, mkurugenzi mkuu wa uvumbuzi wa chapa hiyo ya  "OktobaFest alisema ni sherehe ya utambulisho wa kipekee wa Afrika Mashariki, na safu ya wasanii wa mwaka huu ni dhihirisho la kweli la utofauti wa vipaji vya muziki katika ukanda huu.

Tunayo furaha kuleta pamoja vipaji vya ajabu kama hivi kutoka Sudan Kusini, Tanzania, Uganda, na Kenya na tunatazamia watazamaji kushughulikiwa kwa tajriba zisizosahaulika.

Tamasha hili ni sherehe kubwa ya utamaduni wa Afrika Mashariki, inayoleta watu pamoja ili kufurahia ladha, sauti na tamaduni za kipekee za maeneo yote ya muziki wa Afrika.