logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mchekeshaji Emmanuella aandaa shindano la kula na wanafamilia, ampa mshindi Ksh 30K

Katika klipu hiyo, Emanuella alionekana akiwa na wanafamilia wengine watano.

image
na Davis Ojiambo

Burudani12 October 2023 - 09:36

Muhtasari


  • • Kila mtu kwenye meza alijaribu kadri ya uwezo wake, lakini mmoja wa wajomba wa mtengenezaji wa skit alishinda tuzo ya pesa. Emanuella akamkabidhi zile pesa.
Emmanuella.

Muigizaji wa klipu za ucheshi kutoka Nigeria Emmanuella Samwel amepakia video akionesha jinsi alivyoandaa shindano la mlo na wanafamilia wake ambapo aliweka zawadi kwa mshindi.

Katika klipu hiyo aliyopakia kwenye Instagram yake, mchekeshaji huyo mwenye umri wa miaka 12 anayeigiza na Mark Angel alikuwa amezungukwa na watoto wenzake ambapo kabla ya shindano alitoa masharti ya mchezo huo wa mashindano ya kula.

Katika klipu hiyo, Emanuella alionekana akiwa na wanafamilia wengine watano kwenye meza na sahani za chakula mbele yao.

Alisema kwamba shindano hilo lilikuwa kupima kasi ya kula kwa wanafamilia wenzake na kuwa atakayemaliza wa kwanza kumaliza sinia yake ya chakula angempa dola za Kimarekani 200 sawa na takribani shilingi za Kenya elfu 30.

“Naenda kucheza mchezo wa chakula na wanafamilia wenzangu, mchezo ni kama utakuwa wa kwanza kumaliza chakula chako, nitakupa dola 200. Lakini pia kama ni mimi nitakuwa wa kwanza kumaliza mbele yenu bado nitakula pesa zangu kwa sababu pia mimi ni mshiriki, mko tayari,” Emmanuella aliwauliza wenzake waliokuwa kila mmoja ange na chakula chake kwenye sahani.

Kila mtu kwenye meza alijaribu kadri ya uwezo wake, lakini mmoja wa wajomba wa mtengenezaji wa skit alishinda tuzo ya pesa. Emanuella akamkabidhi zile pesa.

Tazama video hiyo hapa


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved