Burna Boy anavuta bangi nyingi zaidi ya msanii yeyote niliyewahi kutana naye - Ed Sheeran

Hata hivyo, Ed Sheeran alimsifia Burna Boy akisema kwamba anafanya kila kitu kwa ziada si tu katika kuvuta bangi lakini pia katika kutunga mashairi mazuri.

Muhtasari

• "Mimi nilifanya kazi na yeye na naweza sema kwamba huyo ndiye mtu niliona anapenda sana,” alisema.

Ed Sheeran na Burna Boy
Ed Sheeran na Burna Boy
Image: Screengrab

Mwimbaji wa Uingereza Ed Sheeran amefichua kuwa mwanamuziki wa Nigeria Burna Boy ndiye mwanamuziki pekee anayemfahamu anayevuta bangi kila dakika.

Akiongea wakati wa mahojiano, hitmaker huyo wa Perfect alielezea mambo aliyoyaona alipokuwa akifanya kazi na kuzunguka kutoka sehemu moja hadi nyingine na Damini Ogulu maarufu kama Burna Boy.

Alifichua kuwa amefanya kazi na wanamuziki kadhaa kote ulimwenguni lakini hakuna hata mmoja wao anayekaribia Burna Boy linapokuja suala la kuvuta katani ya Hindi kwa sababu yeye huwaongoza wote.

Msanii huyo alizungumza kwamba amefanya kolabo nyingi na wasanii wa kila aina kwa kipindi cha miaka mingi lakini hajawahi kutana na msanii ambaye anapenda kuvuta bangi kama Burna Boy.

Alisema: "Hiyo ndiyo zaidi ambayo nimewahi kuona mtu yeyote akivuta bangi. Mimi nilifanya kazi na yeye na naweza sema kwamba huyo ndiye mtu niliona anapenda sana,” alisema huku akibainisha kwamba Burna Boy anafanya Zaidi katika kila kitu sit u kwenye kuvuta bangi lakini pia kwenye kutunga miziki.

Mwaka mmoja uliopita, wasanii hao wawili waliachia kibao cha pamoja, For My Hand ambapo kilipata ufanisi mkubwa, kwenye mtandao wa YouTube, kibao hicho kina utazamaji wa milioni 123.

Tazama video hii jinsi Sheeran alivyomzungumzia Burna Boy na uzoefu wa kufanya kazi na yeye.