Niliendesha lebo nikiwasimamia wasanii kwa kila kitu miaka 4 bila kufaidi chochote - Davido

Kujitolea kwa Davido kusaidia wengine bila faida ya haraka ya kifedha kulizaa matunda, kwani wasanii kama Mayorkun, Peruzzi, na Dremo walistawi chini ya uongozi wake.

Muhtasari

• Mbali na kueleza mambo haya, Davido kwa sasa anatengeneza documentary ambayo itatoa picha ya nyuma ya pazia kuhusu changamoto alizokutana nazo katika tasnia ya muziki.

Davido
Davido
Image: X

Mwanamuziki wa Nigeria Davido, amefunguka kuhusu siku zake za awali katika tasnia hiyo wakati wa mahojiano ya hivi majuzi na mwanahabari wa Marekani Steve Stoute.

Alifichua kuwa alipoanzisha lebo yake ya Davido Music Worldwide (DMW), aliiendesha kwa miaka minne bila kuchukua pesa kutoka kwa wasanii wake.

Msanii huyo alisema kwamba azma ya kuanzisha lebo yake mara ya kwanza hakuwa na fikira ya kibiashara bali alikuwa tu anajifurahisha na kuwakwamua vijana wasanii kwa kukimu mahitaji yao ya kuachia miziki.

Katika miaka hii ya mwanzo, DMW haikuwa tu lebo; ilikuwa kama familia kwa Davido. Lengo lake kuu lilikuwa kusaidia marafiki zake na wasanii wenzake. Alilipa gharama kama vile utengenezaji wa video, malazi, na ustawi, bila kutafuta faida ya kifedha.

Kadiri mvuto wa kimataifa wa Afrobeats ulivyozidi kuongezeka, Davido alitambua umuhimu wa mbinu yenye mwelekeo wa kibiashara zaidi. Tangu wakati huo amesisitiza hili kwa watia saini wake wapya wa DMW, akiangazia hitaji la kuuchukulia muziki kama biashara na kupata mapato.

Kujitolea kwa Davido kusaidia wengine bila faida ya haraka ya kifedha kulizaa matunda, kwani wasanii kama Mayorkun, Peruzzi, na Dremo walistawi chini ya uongozi wake.

Mbali na kueleza mambo haya, Davido kwa sasa anatengeneza documentary ambayo itatoa picha ya nyuma ya pazia kuhusu changamoto alizokutana nazo katika tasnia ya muziki.

"Unajua mwanzoni, naweza sema niliendesha lebo yangu kwa miaka 4 bila kuchukua kitu chochote, unajua lebo yangu ilikuwa kama muunganiko wa kifamilia, kwangu ilikuwa tu kujifurahisha. nilikuwa nawalipia wasanii wangu kushoot video, na mahitaji mengine," alisema.

Kupitia filamu hii ya hali halisi, analenga kuwatia moyo wasanii wanaochipukia kwa kufichua bidii na azma ambayo ndiyo msingi wa njia yake ya mafanikio.