Kama ni kutumiwa, nilitumiwa na kutemwa-Diana Marua aweka wazi mitandaoni

Diana alisema kuwa alipokutana na Bahati, moyo wake ulihisi tofauti, akaacha kuwaona wanaume wengine wote aliokuwa akitoka nao kimapenzi.

Muhtasari

• Amesimulia safari ya maisha yake ya zamani jinsi wanaume tofauti walivyomtumia kimapenzi na kisha kumtema .

• “Nimekuwa na sehemu yangu ya maisha,kupanda na kushuka. Nimechumbiana na wanaume wa kila aina, nimetumiwa na kutupwa, nimeumia moyoni, lakini wote hawa walikuwa wakinitayarisha kwa mpango wa Mungu,”

Diana Marua/Instagram
Diana Marua/Instagram

Diana Marua amefunguka kuhusu safari yake ya mapenzi ya awali kabla ya kupatana na msanaii Bahati na kuingia kwenye ndoa.

Amesimulia safari ya maisha yake ya zamani jinsi wanaume tofauti walivyomtumia kimapenzi na kisha kumtema  kabla ya umaarufu na pesa, wakati bado hawakuwa wametapatana na Bahati.

Katika video iliyoambatana na ujumbe kwenye ukurasa wake wa Insta, Diana alifichua kwamba alichumbiana na wanaume kadhaa kabla ya kupatana  na Bahati, na na kusema kwamba walimtumia na kumtema.

“Nimekuwa na ukurasa wangu ya maisha,kupanda na kushuka. Nimechumbiana na wanaume wa kila aina, nimetumiwa na kutupwa, nimeumia moyoni, lakini wote hawa walikuwa wakinitayarisha kwa mpango wa Mungu,” alisimulia.

Diana alisema kuwa alipokutana na Bahati, moyo wake ulihisi tofauti, akaacha kuwaona wanaume wengine wote aliokuwa akitoka nao kimapenzi. Alisema amejawa na furaha kwa miaka saba ambayo wamekuwa pamoja, akibainisha kuwa uvumilivu ni muhimu.

"Nilikutana na @BahatiKenya, na niliwaacha wote kwa sababu, mara moja, moyo wangu ulipiga tofauti. Kipindi nilipojua kuwa tunachumbiana, hakuwahi kuniacha. Unaona zawadi unaniona navishwa taji, lakini haya yote yamechukua bidii, uvumilivu, kujitolea, kuomba msamaha unapokosea, tumefuta machozi. kila kitu na kutanguliza hisia za mtu tunapokuwa chini, kutiana moyo hata wakati hatuoni mwanga… orodha ni nyingi sana,” alisema. 

Kwa sherehe ya mahari, alitamani mama yao wawili angekuwapo, akiongeza kuwa wote wanatoka katika familia zilizovunjika.

“Kama ningepewa ombi moja, ingekuwa mama zetu kushuhudia siku hii na kusherehekea nasi 😭 Lakini Mungu alikuwa na mipango mingine. Wanatutazama Mbinguni na najua tumewafanya wajivunie sana. Babe, sote tumetoka kwa familia zilizovunjika lakini asante kwa kuvunja mnyororo huu na unifundishe maana ya kuweka familia na kupigania kila mmoja wakati ulimwengu unatupinga. Umesimama kama kiongozi wa nyumba yetu kwa upendo na heshima nyingi. Ombi langu ni kwamba kwa maisha marefu atushibishe na atuonyeshe wokovu wake,” Diana alisema.