DK Kwenye Beat alichochea taaluma yangu ya uimbaji wa injili - Guardian Angel

"Mafanikio yangu kwenye muziki yaliazishwa na mwanamziki DK nikiwa kidato cha tatu," alisema Guardian Angel.

Muhtasari

• Mafanikio yangu kwenye mziki yaliazishwa na mwanamuziki DK nikiwa kidato cha tatu nakumbuka vizuri walinipeleka Studio wakanilipia ili nirekodi mziki wangu wa kwanza," alisema.

• "Tunaanzisha Lebo ya injili kwa sababu taswira ambayo watu walikuwa nayo kuhusiana na mziki wa injili ilipugua," aliongeza.

DK Kwenye Beat na Guardian Angel.
DK Kwenye Beat na Guardian Angel.
Image: Instagram

Msanii wa  muziki  wa injili wa kizazi kipya, Guardian Angel Alhamisi Oktoba 26 atazindua rasmi lebo yake ya muziki ambayo amekuwa akiijenga kwa muda, Seven Heaven Music.

Kwenye mahojiano ya moja kwa moja na wanablogu wa mitandao msanii huyu alimtaja mwanamziki anayetambulika kama DK Kwenye Beat kama mwazilishi wa muziki wake baada ya kumsaidia kurekodi wimbo  akiwa shule ya upili.

"Mafanikio yangu kwenye muziki  yaliazishwa na mwanamziki DK nikiwa kidato cha tatu nakumbuka walinipeleka Studio wakanilipia ili nirekodi mziki wangu wa kwanza,tangia wakati nilipomaliza shule nilipata mwelekeo wa mziki",alisema.

Guardian Angel kwenye mahojiano haya alisema kuwa nia yake ni kusaidia vijana kufanikisha ndoto zao za mziki kama alivyo fanikishwa na mwanamziki DK kwenye Beat.

Msanii huyo aliweza kutaja sababu ya kuanzisha lebo ya injili wakati huu ambapo wengi wanahisi kwamba watu wengi wanasikiliza miziki ya kidunia,

"Tunaanzisha Lebo ya injili kwa sababu taswira ambayo watu walikuwa nayo kuhusiana na mziki wa injili ilipugua,ndio maana tunajaribu kuchipua kwa sasa Seven Havean ndio mwongozo bora kwa vijana wenye nia ya mziki.