Esther Musila ajilimbikizia sifa kwa kuchangia mafanikio ya Guardian Angel kimuziki

" Nafikiri umahiri wangu katika shughuli za usimamizi ndio umetusaidia kufika pahali tumefika sasa,” Musila aliongeza.

Muhtasari

• “Kwa sasa ninamshukuru Mungu sana kwa vile dunia mzima sasa inamjua ni nani Guardian Angel." alisema.

• "Nafikiri umahiri wangu katika shughuli za usimamizi ndio umetusaidia kufika pahali tumefika sasa,” Musila aliongeza.

Image: INSTAGRAM// GUARDIAN ANGEL

Esther Musila kwa mara nyingize tena amezua mjadala pevu katika mitandao ya kijamii baada ya kudai kwamba kama si yeye, msanii Guardian Angel asingekuwa alipo sasa hivi kimuziki.

Musila alikuwa anazungumza katika uzinduzi rasmi wa lebo ya muziki ya Guardian Angel – Seven Heaven Music – katika hoteli ya Sankara.

Musila alisema kwamba mwanzo alikuja katika maisha ya Guardian Angel kama mpenzi, kisha akawa mchumba kabla ya kufunga harusi na kuwa mke rasmi.

Alikiri kwamba mpaka kufikia hatua ya kuanzisha lebo yake mwenyewe na kuwashika mkono vijana wawili weney talanta, lengo lake limetimia katika maisha ya Guardian Angel, ambaye amepata mabadiliko makubwa chanya tangu walipojuana na kupendana.

“Nafikiri safari yangu, nyinyi wote mnajua jinsi nilivyomkutana huyu jamaa wa ajabu, na niliamini katika ndoto zake. Sifikirii nimewahi amini katika ndoto za mtu kama ambavyo nilifanya kwa Guardian. Kutoka siku ya kwanza nilijua kuna kitu kikubwa ndani yake ambacho kilihitaji kutolewa nje,” Musila alisema kwa sehemu huku akimuangalia Angel kwa mahaba.

“Kwa sasa ninamshukuru Mungu sana kwa vile dunia mzima sasa inamjua ni nani Guardian Angel. Na wajibu wangu, nafikiri nimefanya wajibu wangu. Sijui mengi kuhusu Sanaa ya muziki lakini mimi nilikuja kama mpenzi, mchumba na baadae nikawa meneja. Nafikiri umahiri wangu katika shughuli za usimamizi ndio umetusaidia kufika pahali tumefika sasa,” Musila aliongeza.

Kauli hiyo ilifasiriwa kwa njia tofauti kutoka kwa mahsabiki ambao walihisi alikuwa anajivika koja la maua kwa kumsaidia Guardian Angel huku wengine wakimpa hongera kwa juhudi zake za kuifanya nyota ya Angel kung’aa.

“Inaonekana zaidi kama anajipongeza,” Jakey the Langat alisema.

“Sponsor amesema kila kitu,” Daniel Gits.

“Kuanikwa nayo,” mwingine alisema.